Menu

BASKETBALL: Yaliyojiri NBA weekend hii

………Warriors imeambulia kichapo cha pili katika mechi tatu baada ya kufungwa na Detroit Pistons kwa vikapu 113 kwa 95.
………..Points 38 zilizofungwa na mchezaji nyota Stephen Curry hazikuweza kuisaidia Warriors kuibuka na ushindi katika mchezo huo, huku mchezaji Andre Dummonds kwa upande wa Pistons akiwa ndio mchezaji nyota baada ya kufunga jumla ya points 14 na kuchukua rebounds 21 kuliko mchezaji mwingine yoyote katika mchezo huo.
………….Licha ya kupokea kichapo hicho, bado vijana hao wa kocha Luke Walton wameendelea kuongoza msimamo wa ligi katika conference ya Magharibi baada ya kushinda michezo 37 na kupoteza minne tu katika mechi 41 walizocheza.
…………Huko nako katika conference ya Mashariki, Cleveland Cavaliers anayochezea nyota LeBron James imeendelea kuongoza msimamo hata baada ya ushindi wa jana dhidi ya Houston Rockets wa vikapu 91 kwa 77.
………….Mechi inayofata kwa viongozi hawa wa misimamo, itawakutanisha wao wenyewe siku ya jumanne ya tarehe 19 January katika dimba la Quicken Loans Arena.

Comments

comments

Please follow & like us

Video

Tweets