Menu

CAVALIERS YAANGUKIA PUA MBELE YA WARRIORS, LeBRON JAMES HOI.

Katika kuthibitisha kuwa walifungwa mechi mbili mfululizo kwa bahati mbaya tu, vijana wa kocha Luke Walton, nawazungumzia Golden State Warriors wamethibitisha ubabe wao mbele ya vinara wa Eastern Conference timu ya Cleveland Cavaliers baada ya kuwachapa kwa jumla ya vikapu 132 kwa 98 tena palepale nyumbani kwa Cavaliers, Quicken Loans Arena alfajiri na kuamkia leo.

Wakiongozwa na mkali wao Stephen Curry, Warriors waliingia katika jimbo la Ohio yalipo makazi ya Cavaliers na kuchafulia hali ya hewa uwanjani hapo, huku wengi wakishindwa kuamini kilichotokea kutokana na Warriors kuwa na matokeo mabovu siku tatu za nyuma.

Ilikuwa ni mechi yenye upinzani si tu kwa timu, bali hata kwa wachezaji binfsi huku Stephen Curry akionyeshana uwezo na Mmarekani mwenzake LeBron James, lakini mwisho wa siku alikuwa ni Curry aliyeweza kuondoka na ushindi baada ya kufunga jumla ya points 35, kuchukua rebounds 5 na kutoa assists 4 dhidi ya points 16, rebounds 5 na assists 5 za LeBron. Licha ya Curry, Warriors pia iliweza kubebwa na mchezaji Andre Iguuodala aliyefunga jumla ya points 20

Licha ya matokeo hayo, bado Cavaliers anaongoza msimamo wa Eastern Conference licha ya kufungwa mechi 11 mpaka sasa huku wababe Warriors nao wakiongoza msimamo wa Western Conference.

Comments

comments

Please follow & like us

Video

Tweets