Menu

DAREVA YATANGAZA KOZI YA UKOCHA.

Chama cha mpira wa wavu mkoa wa Dar es salaam (DAREVA) kupitia mwenyekiti wake wa kamati ya ufundi Ndugu Nasoro Sharifu kimetangaza kozi ya Ukocha ya ngazi daraja la kwanza (Level One)kwa wapenzi wa mchezo huo ambao ni wakazi wa jiji la Dar es Salaam tu, ambayo itakuwa ikiongozwa na mtaalam Fredy Mshangama.

Kozi hiyo ambayo itakuwa ikitolewa kuanzia Tarehe 2-10 mwezi February mwaka huu kwenye viwanja vya Jakaya Kikwete Youth Park, itakuwa ikigharimu kiasi cha Tzsh 30,000 kwa kila mtu atakayekuwa tayari kushiriki na kiasi hicho cha pesa kitalipwa siku hiyo ya kuanza kozi ambapo ndipo usajili utafanyika kwa washiriki wote.

DAREVA inatoa wito kwa wapenzi wa mpira wa wavu mkoa wa Dar es Salaam kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya kuchangamkia fursa hiyo adimu katika kufikia kilele cha maendeleo ya mchezo huo hapa mkoani na nchini Tanzania kwa ujumla.

“Watu wajitokeze kwa wingi kwasababu hii ni kozi ambayo inatoka kwenye ngazi ya mkoa ila mafunzo yake ni ngazi ya kimataifa na tunahitaji sana watu wengi hasa hasa wale wanaokaa na watoto muda mrefu kama walimu wa shule za msingi na Sekondari lakini pia watu wanaotarajia kuwa na timu za mitaani kwani itasaidia sana kukuza Volleyball kwa mkoa wetu huu na Tanzania kwa ujumla endapo kama jinsia zote zitajitokeza,” Anaongeza Nasoro Sharifu, Mwenyekiti wa kamati ya ufundi DAREVA.

Comments

comments

Please follow & like us

Video

Tweets