Menu

TANZANIA KUSHIRIKI MASHINDANO YA HOCKEY YA AFRIKA KWA VIJANA

Timu za Tanzania za vijana za mpira wa magongo maarufu kama Hockey zinatarajiwa kushiriki katika mashindano ya mataifa bingwa ya Afrika kwa mchezo huo chini ya miaka 21, mashindano ambayo yatafanyika jijini Windhoek, Namibia kuanzia tarehe 18-28 mwezi March mwaka huu.

Akithibitisha ushiriki huo, katibu wa chama cha mpira wa magongo Tanzania (THA), Kaushik Doshi amesema kwamba Tanzania imethibitisha kupeleka timu katika mashindano hayo kwa jinsia zote mbili za kike na kiume.

Kwa upande wa maandalizi, Doshi amesema kuwa wamekuwa na program ya kukusanya vipaji ambavyo vilionekana kwwenye mashindano ya Mapinduzi na pia wamefanya majaribio kwa vijana kutoka mikoa ya Arusha, Moshi, Tanga, Dar es Salaam na Lindi ambapo wachezaji waliochaguliwa kwenye majaribio hayo walipewa mafunzo ya ziada ya mchezo huo.

Katika mashindano hayo yanayoandaliwa na chama cha mchezo huo wa mpira wa magongo barani Afrika nchi mbalimbali zitashiriki ambapo mpaka sasa nchi zilizothibitisha ni pamoja na Afrika Kusini, Kenya, Misri, Ghana, Nigeria, Namibia, Zimbabwe, Botswana, Zambia na Tanzania ambapo bingwa wa mashindano hayo ataliwakilisha bara la Afrika katika mashindano ya dunia yatakayofanyika New Delhi nchini India Desemba mwaka huu.

Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa Tanzania kushiriki katika mashindano hayo huku wito ukitolewa kwa makampuni kushirikiana na chama cha mchezo huo hapa nchini katika kujitokeza kuzidhamini timu hizo za taifa za vijana ili ziweze kufanya vizuri katika mashindano hayo kwani timu ina wachezaji wenye vipaji vya hali ya juu na wapo tayari kupambana.

Comments

comments

Please follow & like us

Video

Tweets