Menu

CHELSEA VS MANCHESTER UNITED KATIKA PICHA.

Mlinda mlango wa Manchester United David De Gea akiokoa mchomo langoni kwake uliopigwa na beki Branslav Ivanovic wa Chelsea.

Mlinda mlando wa Chelsea Thibaut Courtois akiokoa mchomo wa hatari uliopigwa langoni kwake na mshambuliaji Anthony Martial wa Manchester United

Mlinzi wa kati wa Chelsea Kurt Zouma akiugulia kwa maumivu makali baada ya kutua chini vibaya alipokuwa ameruka hewani kucheza mpira. Hata hivyo Zouma hakuweza kuendelea na mechi baada ya kutolewa nje na nafasi yake kuchukuliwa na Gary Cahill

Mshambuliaji wa Manchester United, Jesse Lingard akifunga bao la kuongoza kwa staili ya aina yake mbele ya walinzi wa Chelsea ambao walishindwa kumzuia na kuruhusu mpira kujaa kimiani ukimuacha mlinda mlango Thibaut Courtois akiwa hana la kufanya.

Mshambuliaji wa Chelsea Diego Costa akimkoromea mshika kibendela baada ya kutokubaliana na maamuzi yake katika mchezo dhidi ya Manchester United kwenye uwanja wa Stamford bridge hapo jana

Mshambuliaji wa Chelsea Diego Costa akiipangua ngome ya Manchester United kabla ya kufunga bao la kusawazisha katika dakika za nyongeza na kufanya mpira kumalizika kwa sare ya 1-1 hapo jana.

Wachezaji wa Manchester wakishangilia goli la kwanza lililofungwa na mshambuliaji Jesse Lingard (35) na kuwapa uongozi katika mchezo huo uliopigwa hapo jana katika dimba la stamford Bridge.

Mshambuliaji wa Chelsea Diego Costa akishangilia mbele ya mashabiki wake baada ya kuifungia timu yake bao la kusawazisha katika dakika za nyongeza na kufanya matokeo kuwa 1-1 katika dimba la Stamford bridge hapo jana

Mlinda mlango wa Manchester United akidaka kwa ustadi mkubwa mpira wa kichwa uliopigwa na kiungo Nemanja Matic wa Chelsea kufuatia kona iliyochongwa na Willian hapo jana katika dimba la Stamford Bridge.

Comments

comments

Please follow & like us

Video

Tweets