Menu

KUELEKEA PAMBANO LA WATANI WA JADI JUMAMOSI HII…..

Bila shaka ukiwa shabiki wa soka hapa Tanzania, basi kuna vilabu vikubwa viwili kama sio vitatu ambavyo miongoni mwao, ndipo mapenzi yako ya dhati yalipo.

Tarehe 20 mwezi huu siku ya jumamosi kutakuwa na mpambano wa watani wa jadi Simba na Yanga katika uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam ikiwa ni raundi ya pili ya ligi kuu soka Tanzania bara na itakuwa ni mechi ya 20 kwa upande wa Simba na ya 19 kwa upande wa Yanga.

Kwenye mzunguko wa kwanza timu hizi zilipokutana, Yanga aliweza kuchomoza na ushindi na mabao 2-0 huku ikiwa ni timu ya kwanza kuifunga Simba kwa msimu huu.

Mpaka sasa Simba anaongoza msimamo wa ligi akiwa na pointi 45 akifuatiwa na Yanga mwenye pointi 43 na mchezo wa Jumamosi utakuwa wenye presha ya hali ya juu maana Simba atataka kutumia nafasi hiyo kuwadhihirishia wadau wa soka kuwa mwaka huu amejipanga kurudi kwenye michuano ya kimataifa huku nayo Yanga ikitaka kurudi kileleni mwa ligi.

 

AMIS TAMBWE VS HAMIS KIIZA

Ukiachana na tambo hizo za watani wa jadi, lakini kumekuwa na kitu kingine ambacho kinaongeza ladha ya pambano hilo ambapo washambuliaji wawili wa kutumainiwa na vilabu hivyo ambavyo kwa misimu tofauti, kila mmoja amewahi kucheza katika vilabu vyote hivyo viwili, yaani nawazungumzia Amis Tambwe wa Yanga ambaye aliwahi kucheza Simba na Hamis Kiiza wa Simba ambaye alishawahi kucheza Yanga.

Tambwe amekuwa akiongoza kwenye mbio za ufungaji magoli kwa muda mrefu sasa tangu kuanza kwa msimu na kabla ya mechi za weekend hii, wawili hawa walikuwa na magoli 14 kila mmoja lakini Hamis Kiiza akatumia vyema nafasi ya Tambwe kutocheza mchezo wa 20 akiwa na Yanga ambapo alikuwa kwenye mashindano ya klabu bingwa barani Afrika,huku yeye akitumbukiza kambani magoli mawili dhidi ya Stand United na kufikisha jumla ya magoli 16 na kukaa juu ya Tambwe.

Wawili hawa wamekuwa nguzo imara kwa timu zao na wamefanya mambo makubwa hali inayowafanya kupendwa zaidi na mashabiki wao.

Sasa umefika wakati wa mashabiki kuchagua nani ni zaidi kati ya wawili hawa bila kujali itikadi za timu na uzuri ni kwamba wawili hawa wameshawahi kucheza timu zote hizi mbili.

Kabla ya kuelekea kwenye pambano la watani wa jadi ambalo litawakutanisha washambuliaji hawa, Nani ni mkali zaidi ya mwenzie?

Tupia kura yako kwa kucomment jina la mchezaji huyo

Je, ni AMISS TAMBWE (yanga) au HAMIS KIIZA (simba)?

Comments

comments

Please follow & like us

Video

Tweets