Menu

“NADHANI NITARUDI ULINGONI HATA BAADA YA KUSTAAFU”, ASEMA PACQUIAO

Mpiganaji masumbwi raia wa Ufilipino, Manny Pacquiao amesema kuwa yupo tayari kustaafu baada ya mechi yake inayofuata ingawa anaweza kurudi ulingoni hata baada ya kustaafu.

Bondia huyo mwenye umri wa miaka 37 alitangaza mwezi Januari kuwa pambano lake lijalo dhidi ya Mmarekani Timothy Bradley litakalochezwa Las Vegas nchini Marekani April 9 litakuwa ni pambalo lake la mwisho huku akitaka kujikita zaidi kwenye siasa za nchini mwake Ufilipino japokuwa hana uhakika kama kustaafu huko kutakuwa kwa moja kwa moja.

“Ni vigumu kusema kwa sasa japokuwa nimeshaamua kuwa baada ya pambano hilo ntastaafu lakini ni vigumu kusema hivyo kwa sababu naupenda mchezo huu na upo karibu zaidi na mimi”. Alisema Pacquiao.

Hata hivyo alipoulizwa kuhusu uwezekano wa yeye kutaka kulipa kisasi dhidi ya Mmarekani Floyd Mayweather, bingwa huyo wa dunia katika uzito wa aina nane tofauti alisema hawezi kujua nini kitatokea lakini hadhani kama atastaafu mojamoja, huku kauli hiyo ikiwafanya wapenzi wa mchezo wa ngumi duniani kuamini kuwa kuna uwezekano wa kuwepo pambano la marudiano kati ya Pacquiao na Mayweather kwa siku za baadaye.

Pambano kati ya Floyd Mayweather na Manny Pacquiao lililochezwa mwaka jana lilivunja rekodi ya mapato katika mchezo huo wa masubwi ambapo liliingiza kiasi cha dola za kimarekani milioni 600 ambapo pia liliweza kuongeza umaarufu wa Mfilipino huyo ambaye safari yake ilianza akiwa kama mtoto wa mtaani na hatimaye kuja kuwa bilionea mwanamichezo hali ambayo imeleta matumaini na hamasa kubwa kwa mamilioni ya watu masikini katika nchi yake ya Ufilipino.

 

 

 

 

Comments

comments

Please follow & like us

Video

Tweets