Menu

SIMON MSUVA (yanga) VS IBRAHIM AJIB (simba), NANI MKALI?

Wawili hawa wanacheza katika vilabu viwili hasimu kwenye nchini Tanzania yaani Simba na Yanga, na wamekuwa na mchango mkubwa katika timu zao.

Kinachowafananisha nyota hawa wawili ni nafasi wanayocheza ambayo ni ya ushambuliaji ambapo aina yao ya uchezaji imekuwa ni kushambulia kutokea pembeni mwa uwanja.

Wawili hawa wana kasi, uwezo wa kuchezea mpira na kikubwa zaidi ambacho kinawafanya wawe mahiri zaidi ni uwezo wao wa kufunga ambapo mpaka sasa Ibrahim Ajib wa Simba ameshafunga magoli 9 kwenye ligi kuu soka Tanzania Bara huku naye Simon Msuva wa Yanga naye akiifungia timu yake magoli 6.

Wakati tukielekea kwenye mpanbano wa watani wa jadi jumamosi wiki hii, wawili hawa wamekuwa gumzo mitaa huku kila timu ikitamba kwamba mchezaji wake atafanya maajabu siku hiyo.

JE, NANI MKALI KATI YAO?

Comments

comments

Please follow & like us

Video

Tweets