Menu

MABONDIA 18 WAITWA KUUNDA TIMU YA TAIFA

Wachezaji 18 wamechaguliwa kuunda timu ya taifa ya ngumi za ridhaa kwa ajili ya kujiandaa na mashindano mbalimbali ya kimataifa yakiwemo ya kufuzu Olimpiki yatakayofanyika Yaounde, Cameroon Macho 9-20 mwaka huu kuelekea kwenye mashindano ya Olimpiki ya Rio 2016 yatafanyika Agosti mwaka huu nchini Brazil

Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa na Shirikisho la ngumi Tanzania (BFT), wachezaji hao wataingia kambini kujiandaa na mashindano ya kuwania kufuzu Olimpiki ya Rio. Pamoja na wachezajia hao, pia wameorodheshwa walimu watakaoifua timu hiyo ya taifa

Wachezaji wanaounda kikosi hicho ni Said Jabiri (Ngome), Mustafa Amri (Kawe) uzani wa 49. Light fly weight ni pamoja na Said Omar (Kigoma), George Costantino (Ngome) uzani wa 52 Fly Weight, Hamad Furahisha, Hamduni Issa (JKT) uzani wa Bantam weight na Isamil Galiatano (Ngome), Mwalami Salumu (Temeke) na Nasa Mafuru (Magereza) uzani wa 60 Light weight.

Wengine ni Kevin Kipinge (Ngome) na Adam Hassan (JKT) uzani wa 64 Lightwelter weight, Selemani Kidunda (Ngome) uzani wa 69 Welterweight, Joseph Peter (Ngome) na Moses John (Kigoma) uzani wa 75 Middle weight.

-BINGWA

Comments

comments

Please follow & like us

Video

Tweets