Menu

IP SPORTS-VOLLEYBALL YAANZA VYEMA KLABU BINGWA DAR.

Timu ya mpira wa wavu(volleyball) ya IP Sports imeyaanza vyema mashindano ya Klabu bingwa mkoa wa Dar hatua ya mchujo hapo jana baada ya kuibamiza timu ya Mgeninani kwa seti 3-0 za 25-18, 25-20 na 25-23 kwenye mechi ya ufunguzi iliyopigwa katika viwanja vya Chang’ombe TTC na kujiweka katika mazingira mazuri ya kufuzu kwa hatua inayofuata.

ArZRhBPJIz7h9CpQ217tfnoCiEeogM1vT4blUVbvio5w (1)

IP Sports ( Jezi za Bluu) VS Mgeninani (Jezi za njano)

 

IP Sports walifanikiwa kuuanza mchezo kwa kasi na kuutawala kwa kiasi kikubwa wakimtumia mchezaji wao mzoefu Shukuru Ally ambaye alikuwa mwiba kwa timu pinzani. Licha ya upinzani mkubwa kutoka kwa Mgeninani lakini hawakuweza kufurukuta na mpaka mchezo unakamilika IP Sports ndio waliibuka washindi.

AosCbUV6Fkv5cHLMWtwuhYBPPlwcYYsNonPRPIyqSfo3

Katika mchezo mwingine uliopigwa hapo jana kwenye viwanja hivyo vya TTC, timu kutoka Tabata Kinyerezi ilifanikiwa kujinyakulia pointi zote tatu baada ya mpinzani wale Dar VCB kutotokea uwanjani.

Mechi hizo zitaendelea tena leo ambapo IP Sports watakuwa wakipambana na Dar VCB huku nao Mgeninani wakikwaana na Tabata Kinyerezi.

At0nFSH-kI58fol1yrSgcMWG68QlMAqV3M2kiaYlfKCI

IP Sports wakishangilia baada ya ushindi

 

Timu nne za juu katika ligi hii ndogo yenye jumla ya timu nane zitafuzu kwa ajili ya kucheza ligi kubwa ya Mkoa wa Dar ambayo itaanza tarehe 9 mwezi April ikiwa ni siku nne tangu kumalizika kwa ligi hii ndogo.

 

Picha kwa hisani ya Sports Eye.

Comments

comments

Please follow & like us

Video

Tweets