Menu

KUOGELEA KWENDA DUBAI KUSAKA TIKETI YA OLIMPIKI

Wachezaji wanne wa kuogelea wanatarajiwa kwenda Falme za Kiarabu kushiriki mashindano ya kimataifa ya Dubai ya kusaka kufuzu Olimpiki Rio yatakayofanyika Machi 29 hadi April 7, mwaka huu

Katibu Mkuu wa Chama cha Kuogelea Tanzania (TSA), Ramadhan Namkoveka alisema mashindano hayo yatawaweka katika nafasi nzuri kwa kuwa yatashirikisha waogeleaji bora na mahiri duniani

Namkovela alisema mashindano yatafanyika katika viwanja vya michezo vya Hamdan Sport Complex na kutakuwa na michezo tofauti na aliwataja wachezaji ambao watakwenda kushiriki mashindano hayo kuwa ni Hilal Hilal, Collins Saliboko, Aliasgher Karimjee na mcheza pekee wa kike, Sonia Tumiotto.

ham

Hamdan Sports Complex

 

Alisema wachezaji hao ni miongoni mwa waliofanya vizuri katika mashindano ya kutafuta klabu bingwa nchini kwa mchezo huo ambapo wachezaji hao waliweza kuvunja rekodi mbalimbali za Taifa.

“Tunaamini kuwa waogeleaji wetu wataweza angalau mmojawapo kufuzu katika tukio moja, hasa ukiangalia matokeo yao ya mashindano ya taifa” alisema

Namkoveka alisema changamoto iliyopo ni kwamba hawana wadhamini wa kuipeleka timu Dubai, kwani wanahitaji Sh Milioni 21 kwa ajili ya tiketi ya ndege, malazi, chakula, tracksuit, nguo za kuogelea pamoja na vifaa vingine muhimu wakati wa mazoezi na mashindano

-BINGWA

 

Comments

comments

Please follow & like us

Video

Tweets