Menu

NIGERIA VS EGYPT: ZIJUE DONDOO MUHIMU KUHUSIANA NA WABABE HAO.

MUDA WA MECHI

Mchezo huo mkubwa kabisa barani Afrika utachezwa katika jiji la Crocodile City of Kaduna nchini Nigeria kuanzia majira ya Saa moja kamili usiku kwa saa za Afrika Mashariki ambapo mechi ya marudiano itapigwa Jumanne ya wiki ijayo kwenye jiji la Alexandria huko nchini.

 

 

MSIMAMO KUNDI G

Wababe hawa wamepangwa kundi G pamoja na timu za Tanzania na Chad katika michezo ya kufuzu kwa kombe la dunia yatakayofanyika mwakani kule nchini Gabon ambapo Misri anaongoza kundi akiwa na alama sita baada ya kushinda michezo miwili ya awali dhidi ya Tanzania na Chad huku Nigeria naye akishika nafasi ya pili baada ya kushinda mchezo dhidi ya Chad na kutoka sare ya bila kufungana na Tanzania.

 

REKODI YA KUTOFUZU AFCON

Timu zote hizi zitacheza mchezo wa leo zikiwa na kumbukumbu mbaya ya kutofuzu katika michuano hii ambapo Nigeria hakufuzu katika michuano iliyopita licha ya kuwa bingwa mtetezi wakati hali ikiwa ni mbaya zaidi kwa Misri ambao hawajashiriki fainali hizi kwa vipindi vitatu mfululizo.

 

UBINGWA WA AFRIKA (AFCON)

 

Misri ndiye bingwa wa kihistoria wa Afrika baada ya kushinda taji hilo mara saba huku mara ya mwisho ikiwa ni mwaka 2010 kule nchini Angola huku naye Nigeria ametwaa taji hilo mara tatu huku mara ya mwisho ikiwa ni mwaka 2013 pale nchini Afrika Kusini

 

MECHI WALIZOKUTANA

Timu hizi zimekutana mara 15 ambapo Misri ameshinda michezo 7 kati ya hiyo huku naye Nigeria akishinda michezo 4 na kutoka sare mara 4. Mchezo wa kwanza kuwakutanisha wababe hawa ilikuwa Januari 1 mwaka 1960 katika mchezo wa kirafiki ambapo Nigeria alishinda 2-1 na mchezo wa mwisho kuzikutanisha timu hizi ilikuwa ni tarehe 12 januari mwaka 2010 ambapo Misri aliibuka na ushindi wa mabao 3-1 huku kipigo kizito baina ya timu hizo mbili ilikuwa ni Novemba 24 mwaka 1963 ambapo Misri alishinda 6-3

Comments

comments

Please follow & like us

Video

Tweets