Menu

VIDEO: YALIYOJIRI MECHI ZA KIRAFIKI NA ZILE ZA KUFUZU HAPO JANA

SUAREZ ARUDI KWA KISHINDO, APIGA MBILI URUGUAY IKITOKA SARE YA 2-2 NA BRAZIL

Luis Suarez aliifungia Uruguay mabao mawili ya kusawazisha dhidi ya Brazil kwenye mechi za kufuzu kwa kombe la dunia hapo jana ikiwa ni mechi yake ya kwanza tangu amalize adhabu yake ya kumg’ata Giorgio Chiellin kwenye fainali za kombe la dunia mwaka 2014 kule nchini Brazil. Tazama Hapa…

UFARANSA YAIONGEZEA MACHUNGU UHOLANZI, YAICHAPA 3-2

Wakati taifa la Uholanzi likiwa kwenye majonzi makubwa ya kuondokewa  na nguli wao wa soka, Johan Cruyff, Jana walikubali kichapo cha mabao 3-2 mbele ya waandaaji wa fainali za mataifa ya Ulaya, Ufaransa katika mchezo wa kujipima nguvu. Tazama hapa..

NIGERIA YASHINDWA KUTAMBA NYUMBANI

Nigeria imejikuta katika wakati mgumu baada ya kushindwa kupata ushindi katika uwanja wake wa nyumbani na kujikuta wakilazimishwa sare ya kufungana goli 1-1 na Misri kwenye mchezo wa kufuzu kwa fainali za mataifa ya Afrika. Bao la kusawazisha la Misri lilifungwa dakika za nyongeza na mshambuliaji Mohamed Salah. Tazama hapa..

RONALDO AKOSA PENATI URENO IKILALA KWA BAO 1-0 MBELE YA BULGARIA

Cristiano Ronaldo alishindwa kuisaidia timu yake ya taifa ya Ureno kuondoka na kipigo katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Bulgaria baada ya mkwaju wake wa penati kuokolewa na kipa Vladislav Stoyanov wa Bulgaria. Goli la Bulgaria lilifungwa na Marcelinho.

Comments

comments

Please follow & like us

Video

Tweets