Menu

HARRY KANE NA JAMIE VARDY WAICHACHAFYA UJERUMANI

Timu ya taifa ya Uingereza maarufu kama Three Lions imefanikiwa kuwabwaga mabingwa wa kombe la dunia wa mwaka 2014, timu ya taifa ya Ujerumani kwa mabao 3-2 katika mchezo wa kirafiki uliochezwa kwenye dimba la Olympia Stadion nchini Ujerumani.

Ujerumani walikuwa wa kwanza kupata bao mnamo dakika ya 43 ya mchezo kufuatia shuti kali lililopigwa na Toni Kroos kabla ya Mario Gomez kuongeza la pili kwa kichwa katika dakika ya 57.

Dakika nne baadae, Harry Kane aliipatia Uingereza bao la kwanza baada ya kuwazunduka walinzi wa Ujerumani ndani ya penati boksi na kuachia mkwaju uliomshinda kipa Manuel Neuer.

Jamie Vardy aliiandikia Uingereza bao la kusawazisha dakika ya 74 baada ya kumalizia vyema krosi ya Nathan Clyne kutoka mashariki mwa uwanja na Eric Dier alimaliza shughuli kwa upande wa Uingereza baada ya kumalizia vyema kwa kichwa mpira wa kona.

TAZAMA HAPA:


 

Comments

comments

Please follow & like us

Video

Tweets