Menu

VIDEO: RONALDO AFUTA REKODI YA BARCELONA YA KUTOFUNGWA MECHI 39.

Cristiano Ronaldo alifunga bao la ushindi kwa Real Madrid ambao walikuwa kumi katika dimba la Camp Nou ambalo jana liligubikwa na huzuni ya kumbukumbu ya nguli Johan Cruyff huku wakitokea nyuma na kumaliza rekodi ya kutofungwa mechi 39 waliyokuwa nayo Barcelona

 

Gaerald Pique alifunga bao la uongozi kwa wenyeji kwa bao safi la kichwa  lakini Karim Benzema alifunga bao la kusawazisha kabla ya Ronaldo kufunga bao la ushindi zikiwa ni dakika tano tu tangu Sergio Ramos kutolewa nje kwa kadi nyekundu

Kwa matokeo hayo sasa, Real Madrid wameipunguza Barcelona kasi kutoka kwenye tofauti ya pointi 10 hadi 7 huku Real madrid ikiendelea kushikilia nafasi ya tatu chini ya Atletico Madrid ambayo nayo jana ilimtandika Real Betis mabao 5-1

MSIMAMO WA LA LIGA BAADA YA MECHI ZA JANA.

MSIMAMO

 

 

 

Comments

comments

Please follow & like us

Video

Tweets