Menu

SAVIO NA VIJANA QUEENS ZATWAA UBINGWA WA KIKAPU MKOA WA DAR

Timu ya mpira wa kikapu ya Savio wanaume imeibuka bingwa wa michuano ya Ligi ya Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam baada ya kuwafunga wapinzani wao Vijana kwa jumla ya vikapu 66 na 59 katika mchezo wa fainali uliochezwa Uwanja wa Ndani wa Taifa Dar es Salaam.

Katika mchezo huo uliokuwa na upinzani wa hali ya juu, Vijana ndio walioongoza kwenye kota ya kwanza kwa vikapu 15 huku Savio wakifunga vikapu 13

Savio walizinduka katika ya pili na kuongoza kwa vikapu 11 dhidi ya nane walivyopata vijana na Kota ya tatu Savio waliendelea kutamba kwa kufunga vikapu 18 dhidi ya tisa vya wapinzani wao.

Katika kota ya nne Vijana walizinduka na kuwazidi wapinzani wao kwa kuwafunga vikapu 27 huku Savio wakifunga 24.

Kwa upande wa wanawake, timu ya Vijana Queens iliibuka bingwa baada ya kuifunga Prisons jumla ya vikapu 69 kwa 63. Katika michuan hiyo, Semeni Aswile wa Prisons aliibuka mchezaji bora upande wa wanawake huku Roma Anania akishinda kwa upande wa wanaume.

Comments

comments

Please follow & like us

Video

Tweets