Menu

REAL MADRID MIKONONI MWA WOLFBURG NDANI YA BERNABEU USIKU WA LEO,

Real Madrid wanakabiliwa na mlima mkubwa wa kupanda katika mechi ya marudiano robo fainali Ligi ya Mabingwa dhidi ya Wolfsburg katika uwanja wa Santiago Bernabeu leo.

Mwendo wa Real Madrid bila kufungwa katika michuano ya Ligi ya Mabingwa msimu huu ulifika mwisho kwani magoli kutoka kwa Ricardo Rodriguez na Maximilian Arnold yaliipatia Wolfsburg ushindi wa 2-0 katika mechi ya kwanza robo fainali iliyopigwa Ujerumani wiki iliyopita ambapo Cristiano Ronaldo alishindwa kuisaidia timu yake kupata hata goli la kufutia machozi pale Ujerumani, Je! usiku wa leo ataweza kujibu mapigo?

CR7, Gareth Bale na Benzema wana jukumu la kufanya kuonyesha ubora wao na thamani ya kubwa katika klabu tajiri Madrid. Ni lazima wathibitishe thamani yao kulinda heshima ya Zidane.

Miamba hao wa Hispania wameshinda mechi zote nne za michuano hiyo msimu huu na wameshinda mechi 22 kati ya 29 walizokutana na klabu za Bundesliga katika uwanja wa nyumbani.

Karim Benzema na Raphael Varane wamerejea mazoezini baada ya kusumbuliwa na majeraha na wanatarajiwa kucheza mechi hiyo. Beki wa kati Sergio Ramos pia amerejea baada ya kuikosa mechi waliyoshinda dhidi ya Eibar kwa adhabu.

Wolfsburg, ambao wanatafuta kutinga nusu fainali ya michuano hii kwa mara ya kwanza wameshinda mechi zao mbili za mwisho ugenini Ligi ya Mabingwa msimu huu.

Daniel Caligiuri hana uhakika wa kucheza katika kikosi cha wageni hao wa Real Madrid kutokana na tatizo la majeraha ya misuli, wakati Sebastian Jung kwa hakika yupo nje ya mchezo.

Zinedine Zidane:

“Tunahitaji kuongeza kiwango chetu – tunatambua dhahiri kwamba tupo nyuma kwa mabao mawili, na tunajua tutacheza mechi tata. Lakini napenda kusema kwamba tunaweza kufanya chochote kufanikiwa.

Msimu huu hatujawa katika kiwango chetu kizuri, lakini bado tunaweza kufanya mambo makubwa. Tunachohitaji kwanza ni kupata nafasi ya kupumzika – kujiandaa vizuri, na hatuna muda wa kutosha. Hatutajichosha sana lakini tutachagua kikosi cha ushindi na mikakati kabambe dhidi ya Wolfsburg. Kuna mambo mengi ya kuzingatia – tunahitaji umakini zaidi.”

Dieter Hecking:

“Tunahitaji kuwatawala Real; tulipambana, tulijitahidi, na tulikuwa na bahati njema na nguvu za kupata ushindi tuliostahili. Tupo katika nafasi nzuri sasa lakini tunajua kitakachotokea katika Madrid.

Tunataka kuonyesha uwezo mkubwa dhidi ya Madrid, tufanye jambo ambalo hakuna anayeweza kudhani inawezekana. Nataka kutinga nusu-fainali.”

 

Comments

comments

Please follow & like us

Video

Tweets