Menu

BELGIUM VS ITALY: MARK CLATTENBURG KUAMUA VITA KATI YA HAZARD NA CONTE

Na Adam Mbwana,

Yamebaki masaa machache kwa miamba miwili ya soka barani Ulaya kumenyana katika mechi yao ya kwanza kundi E la michuano ya Euro 2016 nchini Ufaransa ambapo Ubelgiji watakuwa wakipambana na Italy.

Kabla ya mpambano huu wa leo utakaopigwa kwenye dimba la Parc Olympique Lyonnais jijini Lyon , kuna mambo manne ambayo unatakiwa kuyafahamu ambayo ni:

 

1.MECHI YAO YA SITA KUKUTANA

Mechi hii itakuwa ni ya sita kwa timu hizi mbili kukutana kwenye michuano mikubwa ya soka duniani huku pia ikiwa ni mara ya tatu kwa wawili hao kukutana kwenye hatua ya makundi ya michuano ya Euro ambapo kama utakumbuka mara ya mwisho timu hizo zilikutana kwenye hatua ya makundi ya michuano hii ya Euro mwaka 2000 nchini Ufaransa ambapo Italy aliibuka na ushindi wa mabao 2-0 kutoka kwa Totti na Fiore

 

2. ITALY, UBELGIJI NA SWEDEN NDANI YA KUNDI MOJA TENA WAKIWA UFARANSA PALEPALE

Baada ya miaka 16 kupita, Italy, Ubelgiji na Sweden wanakutana tena kwenye kundi moja la michuano ya Ulaya ambayo inafanyika kwenye ardhi ile ile ya Ufaransa ambapo kwa mara ya mwisho walikutana Mwaka 2000. Watatu hao walipangwa kundi moja (Kundi B) pamoja na timu ya Uturuki, lakini kwa sasa wapo Kundi E pamoja na timu ya Jamhuri ya Ireland. Ni kama Ireland ameingilia ugomvi usimhusu.

 

3. NI EDEN HAZARD VS ANTONIO CONTE

Mechi ya leo itawakutanisha Eden Hazard akiwa kama nahodha wa Ubelgiji na Antonio Conte akiwa kocha wa Italia ambapo wawili hawa watalazimika kuwa maadui kwa dakika 90 wakiwa pande mbili hasimu licha ya ukweli kuwa baada ya mashindano haya kuisha, wawili hawa watakuwa kwenye safari moja kuelekea jijini London kwa ajili ya kuanza kambi ya maandalizi ya msimu ujao wa 2016-17 wakiwa na Chelsea, Antonio Conte akiwa kama kocha mpya na Eden Hazard akiwa kama mchezaji. Urafiki pembeni, ushindi kwanza!

 

4. MARK CLATTENBURG KUAMUA VITA YA HAZARD NA CONTE

Mwisho, Mechi ya leo itachezeshwa na mwamuzi maarufu kutoka nchini Uingereza, Mark Clattenburg ambaye ameshakutana na Eden Hazard uwanjani na pia atakutana na Conte mara nyingi zaidi uwanjani msimu ujao wakiwa kwenye ligi ya EPL. Hivyo Conte ataanza kuizoea ligi ya EPL kwa misimamo ya waamuzi wake akiwa bado nchini Ufaransa.

 

Tukutane Parc Olympique Lyonnais saa nne kamili usiku huu

Comments

comments

Please follow & like us

Video

Tweets