Menu

EURO 2016: UEFA KUZIONDOA MASHINDANONI UINGEREZA NA URUSI

Shirikisho la soka barani ulaya , UEFA, limeonya kuzichukulia hatua na hata kuzifukuza timu za Uingereza na Urusi.

Hatua hiyo ni kufuatia mashabiki wa timu hizo kuwa chanzo cha ghasia zinazotokea kama ambavyo ilitokea wakati wa mechi kati yao ya huko Marseille siku ya juzi.

mashabiki

Suala la ulevi linatajwa kuwa ni moja ya chanzo cha vurugu hizo ambapo baadhi ya mashabiki huenda viwanjani wakiwa wamelewa.

Kufuatia hali hiyo, Waziri wa mambo ya ndani nchini Ufaransa, Bernard Cazeneuve, amewataka waandaaji wa michuano ya Euro 2016 kukataza vilevi katika maeneo ya michezo.

Amesema maeneo ya michezo ni nyeti wakati mechi zikichezwa na hata siku moja kabla ya michuano. Tamko hilo limekuja siku tatu baada ya fujo kuibuka kutoka kwa mashabiki wa Uingereza ma Urusi huko Marseille ambao walikua wamelewa.

Shirikisho la soka barani ulaya,UEFA wameionya England na Urusi kuwa ziko kwenye wasiwasi wa kutolewa katika mashindano ya michuano ya soka barani humo endapo kama mashabiki wao wataendelea kufanya fujo ambapo UEFA wameomba radhi kwa hali ya utovu wa nidhamu zilizojitokeza kati ya urusi na mashabiki wa waingereza huko Marseille

Comments

comments

Please follow & like us

Video

Tweets