Menu

HABARI MPYA: UEFA KUIONDOA URUSI KWENYE MASHINDANO YA EURO 2016

Timu ya taifa ya Urusi imeambiwa na Shirikisho la Soka barani Ulaya UEFA kuwa adhabu watakayoipata endapo wmashabiki wao watafanya vurugu, si nyingine bali ni kuondolewa mashindano

Kauli hiyo ya UEFA imekuja ikiwa ni siku chache kufuatia vurugu zilizofanywa na mashabiki hao katika mchezo dhidi ya England jijini Marseille

russia

Mashabiki wa Russia wakifanya vurugu

Sambamba na adhabu hiyo ya kuondolewa mashindanoni endapo kama matukio hayo yatajitokeza tena, UEFA imeipiga faini ya Euro 150,000 ambayo inatakiwa kulipwa na chama cha soka nchini Urusi

Kundi la mashabiki wa Urusi limefukuzwa nchini Ufaransa kutokana na kujirudiarudia kwa matukio hayo ya vurugu uwanjani ikiwemo ubaguzi pamoja kuwasha moto.

Hata hivyo uamuzi wa adhabu hiyo ya kuondolewa mashindanoni  na faini upo chini ya mamlaka ya bodi za nidhamu za UEFA na milango ya kukata rufaa bado ipo wazi

 

 

Comments

comments

Please follow & like us

Video

Tweets