Menu

HESHIMA: DE ROSSI ASEMA USHINDI WA ITALY JANA UMEWAZODOA WENGI

Kipigo walichokitoa Italy jana kwa Ubelgiji huenda kikawa kimewashtua wengi, na kama wewe ni miongoni mwao hao walioshtuka basi Ujumbe wako huu hapa.
Kiungo wa Italy, Daniele De Rossi anahisi kuwa timu yake inachukuliwa poa kuelekea kwenye michuano ya Euro 2016 lakini hata hivyo kutokana na dozi waliyotoa jana, De Rossi mwenye umri wa miaka 32 anasema kuwa wamewafunga midomo walio wengi
de

Daniele de Rossi

Italy walikuwa wakichukuliwa poa kutokana na kutokuwa na wachezaji wenye majina makubwa kikosini lakini ushindi wa jana umebadili mtazamo.
Kikosi hicho cha kocha Antonio Conte kilionekana kuwa imara zaidi kwenye idara ya ulinzi ambapo waliweza kuzuia mashambulizi ya Ubelgiji ya kina Eden Hazard hususani kipindi cha pili
“Ushindi huu umewaeleza watu kuwa sisi ni timu nzuri. Kabla ya hapo, watu walikuwa wanavizungumzia vikosi vingine na labda tulikuwa tunachukuliwa poa, Lakini kwa sasa, hali hiyo itapungua”, Alisema De Rossi

Comments

comments

Please follow & like us

Video

Tweets