Menu

EURO 2016: ENGLAND VS SLOVAKIA, ROONEY NA WENZIE SITA KUANZIA BENCHI

Nahodha wa England, Wayne Rooney anatarajiwa kupumzishwa na kocha Roy Hodgson kwenye mchezo wa mwisho wa kundi B dhidi ya Slovakia ambapo Jordan Henderson anatarajiwa kuchukua nafasi ya nahodha huyo ikiwa ni moja ya mabadiliko sita yatakayokuwepo kwenye kikosi hicho maaarufu kama Three Lions ambayo ni Daniel Sturridge, Jamie Vardy, Jack Wilshere, Ryan Bertrand na Nathaniel Clyne wakiwapumzisha Dele Alli, Danny Rose, Kyle Walker, Harry Kane na Raheem Sterling ambao walianza katika mechi mbili za kwanza dhidi ya Urusi na Wales

england kikosi

Kikosi cha England kinachotarajiwa kuanza leo dhidi ya Slovakia

England watakuwa na nafasi ya kuibuka vinara wa kundi B endapo kama watapata ushindi usiku wa leo ingawa kitendo cha Hodgson kubadili wachezaji sita kwenye kikosi cha kwanza inaonekana kuwa hatari hususani kwa nafasi ya Rooney ambaye amefanya vyema kwenye nafasi yake mpya ya kiungo.

Lakini hata hivyo uamuzi wa kuwabadilisha Harry Kane na Raheem Sterling na nafasi zao kuchukuliwa na Vardy na Sturridge katika mchezo dhidi ya Wales ambapo walifunga mabao mawili na kuipa timu yao ushindi lilikuwa linatarajiwa katika mchezo wa leo hasa baada ya viwango walivyovionesha

england2

Wachezaji wa England wakiwa mazoezini kujiandaa na mchezo dhidi ya Slovakia

 Ikiwa inafahamika kuwa Dele Ali amechukizwa na kitendo cha Wilshere kuanza badala yake, Beki wa kulia, Kyle Walker ambaye amekuwa na kiwango bora atapumzishwa na nafasi yake kuchukuliwa na Nathan Clyne huku Ryan Bertland akiandaliwa kuchukua nafasi ya Rose

 

Hata hivyo Hodgson alipoulizwa kama atafanya mabadiliko, alisema kuwa haoni umuhimu wa kufanya hivyo kwani wachezaji wapo kwenye hali nzuri

“Haitakuwa tatizo kama nitaamua kuchezesha kikosi kilekile, lakini kuna wachezaji ambao wangependa kucheza na wamekuwa wakinigongea mlangoni wakitaka kucheza”.

“Nina machaguo mengi kwasababu kila mtu anatamani kuonyesha wanachotaka kufanya. Ni swali la kutaka kujua ni nini tunataka kufanya kuliko kuzingatia kipi ni muhimu”, Alisema Hodgson

 

 

 

Comments

comments

Please follow & like us

Video

Tweets