Menu

DOWNLOAD APP YA M-PAPER KUSOMA MAGAZETI YA MICHEZO KWENYE SIMU YAKO

Ikiwa ni katika kuhakikisha kuwa inatekeleza mpango wake wa kuifanya Tanzania kuwa katika mfumo wa kidigitali, Leo hii Kampuni ya Vodacom imetangaza kuwa smartphone zote ikihusisha pia zile ambazo zinaendeshwa na mfumo wa iOS zinaweza kuitumia app ya M-Paper ambayo inawapa nafasi  wateja wake kusoma magazeti na majarida kupitia simu zao kwa nusu ya bei ya magazeti halisi

Kupitia app hii ya M-Paper ambayo imetengenezwa na kampuni ya Smart Codes kwa ushirikiano na Vodacom, huwezi kupitwa na taarifa yoyote ya kimichezo kutoka kwenye magazeti mahususi ya michezo yapatikanayo humo kama vile Dimba, Bingwa, Champion, Spoti Leo tena kwa nusu bei ya ile ya magazeti ya kawaida yaliyochapishwa.

M-Paper inaweza kupakuliwa bure kwenye App store yoyote au mtandaoni kupitia www.mpaper.vodacom.co.tz  ambapo baada ya kuipakua, magazeti au majarida ambayo mteja atachagua kuyasoma yatalipiwa kupitia M-Pesa au muda wa maongezi huku kwa wale ambao wapo nje ya nchi watalipia kupitia kadi zao za malipo au zile za ATM.

eshot 4

Moja ya sifa kuu za app hii ya M-Paper ni pamoja na kuweza kusomwa kwa kutumia lugha mbili za Kiswahili na Kiingereza, Bei yake ni nusu ya bei ya magazeti ya kuchapishwa, pia unaweza kulipia kwa kutumia M-Pesa, salio kupitia muda wa maongezi ya Vodacom, MasterCard, Visa na American Express huku pia magazeti yaliyopakuliwa yanaweza kusomwa bila ya msomaji kuwa online lakini pia unaweza kusoma gazeti ukiwa mahali kokote duniani na muda wowote

Jikamatie magazeti yako ya michezo uyapendayo kama vile Bingwa, Dimba, Champion na Spoti Leo kupitia smartphone yako mahali popote ulipo na muda wowote uutakao kila siku ili usipitwe na taarifa yoyote ya michezo kupitia app ya M-Paper.

 

Comments

comments

Please follow & like us

Video

Tweets