Menu

BALE AONGOZA ORODHA YA WACHEZAJI BORA EURO 2016 HATUA YA MAKUNDI

Kura zilizopigwa na wasomaji wa mtandao wa Goal zinaonesha kuwa winga wa timu ya Wales, Gareth Bale amewashinda Andres Iniesta, Michal Pazdan na Dimitri Payet na kuwa mchezaji bora wa hatua ya makundi katika michuano ya Euro 2016
Winga huyo Real Madrid amekuwa ni mchezaji pekee kufunga mechi zote tatu za hatua ya makundi na kuisaidia timu yake kutinga hatua ya 16 bora
Bale amepata asilimia 27 za kura zote akimshinda Michal Pazdan (21%) ambaye amekuwa ni nguzo imara kwenye safu ya ulinzi ya Poland ambayo mpaka sasa haijaruhusu bao hata moja tangu kuanza kwa mashindano hayo
Shujaa wa Ufaransa, Dimitri Payet alipata asilimia 21 ya kura akiwa ametupia kambani magoli mawili dhidi ya Romania na Albania kutoka kundi A
payet

Dimitri Payet (Ufaransa)

Wachezaji wengine ambao walipigiwa kura ni pamoja na Andres Iniesta  kutoka Hispania aliyepata asilimia 12 ya kura zote aking’aa kwenye michezo dhidi ya Jamhuri ya Czech na Uturuki.

Naye nahodha wa Croatia, Darijo Srna amepata asilimia 6 ya kura zote huku akionyesha kiwango cha hali ya juu na kuiwezesha Croatia kuongoza kundi D mbele ya Spain licha ya kufiwa na baba yake mzazi.

michal

Michal Pazdan (Poland)

Mlinzi wa Italy, leonardo Bonucci, Kiungo nyota wa Slovakia, Marek Hamsik na mpiga pasi maarufu wa Uswis, Granit Xhaka wote kwa pamoja wamepata asilimia 4 ya kura zotw huku Michael McGovern wa Ireland ya Kaskazini, Alvaro Morata wa Hispania na Jonas Hector wa Ujerumani wakipata asilimia ya 1 ya kura zote kwa kila mmoja wao

Comments

comments

Please follow & like us

Video

Tweets