Menu

UEFA YATANGAZA KIKOSI BORA CHA MASHINDANO YA EURO 2016, URENO YATOA WANNE

Baada ya purukushani za takribani mwezi mzima, hatimaye michuano ya UEFA EURO 2016 imefikia ukingoni usikuwa kuamkia leo huku tukishuhudia URENO wakiibuka mabingwa wapya huku ikiwa ni mara yao ya kwanza kutwaa taji hilo.

Jopo la ufundi la UEFA lilikuwa likifuatilia kwa ukaribu michuano hiyo hatimaye leo limetangaza kikosi cha wachezaji 11 bora wa michuano au kwa lugha nyepesi tuseme ni wachezaji 11 waliofanya vyema zaidi kwenye michuano hiyo na kuwaweka kwenye kikosi kimoja.

Kikosi hicho kimechaguliwa na timu ya wataalamu 13 kutoka UEFA wakiongozwa na Ofisa Mkuu wa Ufundi wa UEFA, Ioan Lupescu huku pia wakiwemo Sir Alex Ferguson, Alain Giresse, David Moyes, Packie Bonner, Mixu Paatelainen, Savo Milošević, Peter Rudbæk, Gareth Southgate, Thomas Schaaf, Jean-François Domergue, Ginés Meléndez na Jean-Paul Brigger.

Wataalamu hao walichagua kulingana na vigezo ambavyo viliainishwa hapo awali kabla ya mashindano kuanza huku mfumo wa uchezaji uliochaguliwa ni ule ambao ulitumika na timu nyingi zaidi kwenye mashindano hayo wa 4-2-3-1 ambapo wataalamu wawili walikuwa wakihudhuria kwenye kila mechi na ripoti zao pia zitachangia kwenye ripoti ya kiufundi ya mashindano ya  UEFA EURO 2016 ambayo itatolewa rasmi kwenye mtandao wa UEFA.com mwezi Septemba.

Kikosi kikiwa katika mfumo wa (4-2-3-1): Rui Patrício (Portugal); Joshua Kimmich (Germany), Jérôme Boateng (Germany), Pepe (Portugal),Raphaël Guerreiro (Portugal); Toni Kroos (Germany), Joe Allen (Wales); Antoine Griezmann (France), Aaron Ramsey (Wales), Dimitri Payet (France); Cristiano Ronaldo (Portugal).

 

best squad

 

 

Comments

comments

Please follow & like us

Video

Tweets