Menu

URENO NDIO MABINGWA WAPYA WA MICHUANO YA EURO 2016

Ureno wamefanikiwa kutwaa ubingwa wa michuano ya Euro 2016 baada ya kuwagaragaza wenyeji Ufaransa kwa bao 1-0 kwenye dimba la Stade de France jijini Paris nchini Ufaransa.

Éderzito António Macedo Lopes maarufu kama EDER aliyeingia kuchukua nafasi ya Renato Sanches dakika ya 79 ya mchezo, ndiye shujaa wa mchezo baada ya kufunga bao la pekee katika mchezo huo wa fainali dakika ya 109 ya mchezo kwa shuti la mbali ambalo lilimshinda golikipa Hugo Lloris baada ya kuguswa na mlinzi Samule Umtiti.

Mambo yalikuwa magumu kwa upande wa Ureno baada ya mchezaji wao tegemeo, Cristiano Ronaldo kuumia kipindi cha kwanza katika dakika ya 24 tu baada ya kugongana na Dimitri Payet dakika ya 7 ya mchezo ambapo nafasi yake ilichukuliwa na Ricardo Quaresma.

Lakini shukrani za pekee zimuendee mlinda mlango wa Ureno, Rui Patricio baada ya kuokoa michomo kadhaa ya washambuliaji wa Ureno kama vile Olivier Giroud, Moussa Sissoko na Antoine Griezmann huku Adre Pierre Gignac akipoteza nafasi ya kufunga dakika za nyongeza kwenye dakika ya 90 za kawaida za mchezo.

Hadi kipenga cha mwisho cha mwamuzi Mark Clattenburg kinapulizwa kuashiria kukamilika kwa dakika 120 za mchezo, Ureno 1, Ufaransa 0 na kuwashuhudia Ureno wakitwaa ubingwa wao wa kwanza wa michuano hii mikubwa kwa ngazi ya timu za mataifa barani Ulaya

 

Comments

comments

Please follow & like us

Video

Tweets