Menu

RIO 2016: RATIBA YA ROBO FAINALI MCHEZO WA SOKA KWA WANAUME HAPO KESHO

Michuano ya Olimpiki huko Rio de Janeiro nchini Brazil imeingia siku ya sita hivi leo ambapo tayari wanamichezo mbalimbali wameshajizolea medali zao huku Marekani akiongoza kwa idadi ya medali, Jumla akiwa medali 38. 16 kati ya hizo zikiwa za dhahabu, 12 za almasi na 10 za fedha.

Kwenye upande wa soka tayari hatua ya robo fainali imeshawadia na hapo kesho timu zitaanza kupepetana.

 

RATIBA KAMILI YA ROBO FAINALI HAPO KESHO:

URENO VS UJERUMANI SAA 1:00 USIKU kwa saa za Afrika Mashariki.

Ureno anaingia kwenye hii akitokea kundi D alipomaliza katika nafasi ya pili nyuma ya Honduras huku nae Ujerumani anatokea kundi C aliposhika nafasi ya kwanza. Mpaka sasa wachezaji wanaoongoza kwa ufungaji mabai ni pamoja ni Nils Petersen na Serge Gnaby ambapo kila mmoja wao amefunga mabao matano huku Ureno nao watakuwa wanaringia mchezaji wao Goncalo Paciencia mwenye magoli matatu

 

NIGERIA VS DENMARK – Saa 4:00 USIKU kwa saa za Afrika Mashariki

Nigeria amemaliza kama kinara wa kundi B huku Denmark nae akimaliza kama mshindi wa pili wa kundi A. Nigeria watakuwa na mchezaji wao mahiri Oghenekaro Etebo aliyepachika mabao manne mpaka sasa hali kadhalika Denmark nao watakuwa na RObert Skov mwenye bao moja.

 

JAMHURI YA KOREA VS HONDURAS – Saa 7:oo USIKU kwa saa za Afrika Mashariki

Jamhuri ya Korea walimaliza katika nafasi ya pili kundi C nyuma ya Ujerumani huku Honduras wakimaliza kama vinara wa kundi D. Korea watakuwa na wachezaji wao mahiri kama vile Chang Hoon Kwon, Suk Hyun Jun na Seung woo Ryu ambao kila mmoja wao amefunga mabao matatu huku Honduras wakijivunia Anthony Lazano mwenye magoli mawili mpaka sasa

 

BRAZIL VS COLOMBIA Saa 10:00 ALFAJIRI kwa saa za Afrika Mashariki

Brazil ameibuka kinara kundi A licha ya kuanza kwa sare mbili mfululizo za kutofungana huku Colombia wenyewe wakimaliza katika nafasi ya pili kundi B nyuma ya Nigeria. Brazil watakuwa wakiongozwa vyema na Gabriel mwenye magoli mawili mpaka sasa na nahodha wao Neymar anayechezea Barcelona huku nao Colombia wakijivunia uwepo wa Teofilo Gutierrez mwenye mabao matatu na Dorlan Pabon mwenye mabao mawili.

Comments

comments

Please follow & like us

Video

Tweets