Menu

KICHUYA AIPA SIMBA POINTI TATU MUHIMU IKIIFUNGA STAND UNITED KWA BAO 1-0

Wekundu wa Msimbazi Simba wameendelea kujikita kileleni mwa msimamo mwa ligi baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya wenyeji wao Stand United kwenye uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.

Bao pekee la wekundu hao wa msimbazi lilifungwa na kiungo mshambuliaji, Shiza Kichuya kwa mkwaju wa penati dakika ya 33 ya mchezo baada ya mshambuliaji Laudit Mavugo kuwekwa chini eneo la hatari na mlinzi wa Stand United.

Kwa matokeo hayo sasa, Simba imefikisha jumla ya alama 35 baada ya kushuka dimbani mara 13 wakiwa wameshinda michezo 11 na kutoa sare miwili tu huku wakiwa hawajapoteza mchezo wowote mpaka sasa na ukiwa ni mchezo wa sita mfululizo kwa golikipa wa Simba, Vincent Angban kucheza bila kuruhusu nyavu zake kutikiswa huku pia akicheza jumla ya michezo 10 bila kuruhusu goli lakini pia bao la leo la Shiza Kichuya linakuwa ni bao lake la tisa tangu kuanza kwa VPL msimu huu na kuongoza orodha ya wachezaji wanaowania kiatu cha ufungaji bora.

Comments

comments

Please follow & like us

Video

Tweets