Menu

VPL 2016: MBEYA CITY YAICHAPA YANGA MABAO 2-1 UWANJA WA SOKOINE HUKO MBEYA

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Soka Tanzania bara timu ya Yanga imekwaa kisiki huko jijini Mbeya baada ya kupokea kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa wenyeji wao Mbeya City mchezo uliopigwa kwenye dimba la Sokoine.

Mbeya City ndio walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya sita tu ya mchezo lililofungwa na Hassan Mwasapili aliyeukwamisha mpira wavuni kwa faulo ya moja kwa moja iliyomshinda golikipa Deogratius Munishi.

Kenny Ally aliiongezea bao Mbeya City dakika ya 35 ya mchezo lililofungwa na Mshambuliaji Kenny Ally bao ambalo lilizua utata hali iliyowafanya wachezaji wa Yanga kumzonga mwamuzi kwa madai kuwa mpira huo ulipigwa bila ya filimbi ya mwamui kuruhusu, lakini hata baada ya mwamuzi kujadiliana na wasaidizi wake wakaruhusu bao hilo hali iliyofanya mashabiki wa timu hiyo kufanya vurugu jukwaani na kuwafanya askari kuingilia kati kutuliza vurugu.

Donald Ngoma alipunguza mzigo wa magoli baada ya kuipatia Yanga goli dakika za nyongeza kuelekea mapumziko baada ya kumalizia kwa kichwa krosi ya Simon Msuva na hadi mpira unakwenda mapumziko, Mbeya City 2, Yanga 1.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi kwa timu zote kufanya mabadiliko na kushambuliana kwa zamu lakini hata hivyo hakukuwa na mabadiliko yoyote katika upande wa matokeo. Na hadi dakika 90 za mchezo zinakamilika, , Mbeya City 2, Yanga 1.

Hicho kitakuwa ni kichapo cha pili kwa timu ya Yanga baada ya kupoteza mchezo wa kwanza dhidi ya Stand United kule mjini Shinyanga na kwa matokeo hayo sasa Yanga wanabaki na pointi zao 27 baada ya kucheza michezo 13.

Comments

comments

Please follow & like us

Video

Tweets