Menu

TETESI ZA USAJILI: MSHAMBULIAJI WA ZESCO ATUA DAR KUSAINI SIMBA

Mshambuliaji Juma Luizio wa Zesco ya Zambia ametua nchini usiku wa kuamkia leo na kuna taarifa zinaeleza anaweza kujiunga na Simba kwa mkopo.

Luizio alikuwa chini ya Kocha George Lwandamina ambaye sasa amejiunga na Yanga.

Taarifa zinaeleza, Luizio amekubali kujiunga na Simba kwa mkopo ili kuboresha kiwango chake.

Mtanzania huyo amekosa namba ya kudumu katika kikosi cha Zesco chini ya Lwandamina.

Hata hivyo taarifa hizo zimekuja mufa mfupi baada ya Simba kukamilisha usajili wa mshambuliaji Pastory Athanas kutokea Klabu ya Stand United.

Comments

comments

Please follow & like us

Video

Tweets