Menu

USAJILI: OSCAR AAGA CHELSEA, PAYET AITAMANI ARSENAL HUKU DEPAY AKIKARIBIA KUTUA EVERTON

Nyota wa klabu ya Chelsea ambaye anahusishwa kujiunga na klabu ya ligi kuu ya nchini China, Oscar, ameshawaaga wachezaji wenzake wa Chelsea kuelekea kwenye usajili huo wa pesa kubwa inayokadiriwa kufika paundi milioni 50.

“Oscar ameshasema kwaheri, Ni rafiki mzuri na mchezaji mzuri. Namtakia kila heri yeye na familia yake. Maisha ya mwanasoka huenda haraka sana na kama ofa kama hiyo ikija unatakiwa uifikirie familia yako. Unatakiwa kujiandaa kwa ajili ya maisha ya baadae ya kustaafu”. Amesema Willian.

 

DEPAY AITAMANI ARSENAL

Dimitri Payet amependekeza kuwa anatamani kujiunga na washika mitutu wa London klabu ya Arsenal licha ya kusisitiza kuwa Arsene Wenger hajawahi kutangaza ofa kwa ajili yake.

Nyota huyo kutoka Ufaransa anayekipiga katika klabu ya West Ham amekuwa akihusishwa na timu mbalimbali katika jiji la London ambapo ripoti mbalimbali zikisema kuwa Wenger anaamini Mfaransa huyo atakuwa na msaada mkubwa kwa Arsenal.

“Nasoma taarifa kuwa Wenger ananichukulia mimi kama mtu nnayekosekana kwenye timu yake lakini hajawahi kuniambia hivyo”, Payet amesema.

 

ROBBEN ANAAMINI DEPAY ATANG’AA AKIWA NA EVERTON

Kinda mholanzi anayekipiga kwenye klabu ya Manchester United, Memphis Depay amekuwa akihusishwa na dili la kujiunga na klabu ya Everton ambayo inafundishwa na mholanzi mwenzake, Ronald Koleman siku za hivi karibuni huku nyota wa Bayern Munich, Aarjen Rooben ambaye pia ni mholanzi akiamini kuwa Depay anaweza kukuza kiwango chake cha kiuchezaji akiwa Everton.

Comments

comments

Please follow & like us

Video

Tweets