Menu

BARCELONA YAINGIA KWENYE KINYANG’ANYIRO CHA KUMUWANIA DIEGO COSTA

Baada ya kuhusishwa na uhamisho wa kuhamia nchini China ambapo atakuwa akilipwa mshahara wa  paundi milioni 30 kwa mwaka, taarifa nyingine zimeibuka na kudai kuwa mshambuliaji wa Chelsea, Diego Costa anatakiwa na klabu ya Barcelona pamoja na Atletico Madrid.

Tovuti ya The Sun ya nchini Uingereza inadai kuwa Barcelona wanataka kutumia mwanya wa mchezaji huyo kutokuwa na maelewano mazuri na waajiri wake kumpeleka Camp Nou ikiwa ni katika mikakato ya kuziba pengo la Luiz Suarez mwenye umri wa miaka 30 kwa sasa.

Nayo Atletico Madrid inasemekana kutaka kumrudisha nyota wao huyo wa zamani ili kuchukua nafasi ya Antonio Griezmann ambaye muda wowote kuanzia sasa anaweza kutua kwenye dimba la Old Trafford ya ada ya uhamisho ya paundi milioni 100.

 

Comments

comments

Please follow & like us

Video

Tweets