Menu

KUTOKA KAMBI YA ARSENAL; HIZI NDIZO TAARIFA NNE ZA USAJILI ZILIZOSHIKA KASI; BENZEMA VEEPE..!!!

1. Alexis Sanchez

Klabu ya Atletico Madrid imemtangazia ofa mshambuliaji wa Arsenal, Alexis Sanchez ambaye wanamuona kuwa ni mrithi sahihi wa Antoine Griezmann.

Wababe hao wa Hispania wanajiandaa kumlipa nyota huyo kutoka Chile mshahara wa paundi 220,000 kwa wiki ambayo ni zaidi ya ile paundi 160,000 aliyowekewa mezani na Arsenal kama akisani mkataba mpya

2. Karim Benzema

Klabu ya Real Madrid imemuweka sokoni mshambuliaji wake Karim Benzema huku vilabu vya Arsenal na Chelsea vikionekana kuwa na nafasi kubwa ya kumtwaa mfaransa huyo

Rais wa Madrid, Florentino Perez anatajwa kuchukizwa na nyota huyo mwenye miaka 29 hususani baada ya mashabiki kumzomea katika mechi yao dhidi ya Real Sociedad.Perez ameviambia vilabu hivyo vya EPL kuwa mshambuliaji huyo yupo sokoni huku pia klabu ya PSG ikionesha nia ya kumtwaa nyota huyo wa zamani wa Lyon.

3. Arsene Wenger

Klabu ya Arsenal ipo kwenye mazungumzo na wawakilishi wa Juventus kuhusu uwezekano wa kumsajili kocha Max Allegri

Wenger bado hajasaini mkataba mpya ambapo Allergi anatajwa kurithi mikoba hiyo mwisho wa msimu.

 

4. Antoine Griezmann

Arsenal wanatajwa kuingia kwenye kinyang’anyiro na Klabu ya Manchester United cha kuiwania saini ya Antoine Griezmann.

United inasemekana kuongoza mbio hizo za kumsajili mfaransa huyo mwenye thamani ya Paundi milioni 85 ambaye alishika nafasi ya tatu kwenye tuzo za mchezaji bora wa dunia mwaka jana.

Arsenal inasemekana kuwa wapo tayari kufikia dau hilo ambalo United walilitaja huku tofauti pekee ikibaki kwenye mshahara ambapo United wameweka ofa kubwa kuliko Arsenal

 

Comments

comments

Please follow & like us

Video

Tweets