Menu

CHELSEA YATAKIWA KUTOA PAUNDI MILIONI 40 ILI KUMNASA MPINZANI WA DIEGO COSTA

Klabu ya Chelsea imeambiwa inahitajika kutoka kiasi cha paundi milioni 40 kwa ajili ya kumnasa mshambuliaji wa Celtic, Moussa Dembele baada ya kutuma ofa ya kushtukiza kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili usiku wa leo

Chelsea wanatakiwa kufanya uamuzi wa haraka kwa Dembele baada ya kuona ofa mbili walizozitegemea za mlinzi Sead Kolasinac na golikipa Craig Gordon zikiwa shakani

Celtic hawana mpango wa kumuuza Dembele mwezi huu lakini tovuti ya Sky Sport inasema kuwa klabu hiyo imewaambia Chelsea kwamba watahitaji kiasi hicho cha pesa kwa ajili ya kinda huyo mfaransa mwenye umri wa miaka 20 waliyemsajili majira ya joto kutokea Fulham

Comments

comments

Please follow & like us

Video

Tweets