Menu

KLABU BINGWA VOLLEYBALL MKOA WA DAR (DAREVA LEAGUE) KUANZA KUUNGURUMA MACHI 5 UWANJA WA NDANI (INDOOR)

Ligi ya vilabu bingwa vya mkoa wa Dar es Salaam kwa mchezo wa mpira wa wavu marufu kama VOLLEYBALL DAREVA LEAGUE  itaanza kuunguruma Tarehe 5 mwezi Machi mwaka huu.

Ligi hiyo inayoandaliwa na Chama cha mchezo huo kwa mkoa wa Dar es Salaam (DAREVA) kwa mwaka huu wa 2017 itajumuisha jumla ya vilabu 10 kwa upande wa wanaume ambazo ni Jeshi Stars (bingwa mtetezi),  Tanzania Prisons, IP Sports, Makongo High School, Mji Mwema, Victory Sports, JKT, Kinyerezi, Police Marine na Chui

Kwa upande wa wanawake timu zitakazoshiriki ligi hiyo yenye upinzani mkali kwa mwaka huu ni tano ambazo ni Jeshi Stars (bingwa mtetezi), Mji Mwema, JKT, Tanzania Prisons na  Makongo High School.

Naye Mkurugenzi wa ufundi wa DAREVA, Ndugu Nassor Sharif, amezikumbusha timu shiriki kumalizia zoezi la usajili wa wachezaji mapema iwezekanavyo kabla ya kuanza kwa ligi hiyo itakayofanyika uwanja wa ndani wa taifa (Indoor Stadium) na Viwanja vya CDS Park Chang’ombe Kuanzia mwezi Machi hadi Agosti mwaka huu.

“Mambo yanaenda vizuri  na pia napenda kukumbusha timu zote zinazo cheza ligi kubwa ya DAREVA mwaka huu kuwa usajili mwisho tarehe 25 mwezi huu yani usiku wa kuamkia kwenye mechi ya  All stars usajili utakuwa umefungwa na sitapokea fomu yoyote ikifika tarehe 26”.

“Fomu zimetolewa muda mrefu na maelekezo yameshatolew naomba zijazwe kila kipengele kama zinavyo elekeza na baada ya kupata fomu za timu zote nitazipiga picha na kuziweka wazi ili watu wote wajue usajili wa kila timu sio siri naomba tujitaidi napokea fomu hata sasa hivi kama zipo tayari zijazwe kote na picha ziwekwe”, Alisisitiza Ndugu Nassor Sharif.

Kabla ya kuanza kwa ligi hiyo Machi 5, itachezwa mechi ya All Stars ambayo itakutanisha kombaini ya timu mbili za wachezaji waliofanya vizuri kwenye mashindano ya mwaka jana ambayo yalimalizika kwa timu za Jeshi Stars wanaume na wanawake kuibuka mabingwa.

Comments

comments

Please follow & like us

Video

Tweets