Arsenal inajiandaa kutuma ofa ya kushtukiza kwa klabu ya Manchester United kwa ajili ya kumnasa kiungo mkongwe, Michael Carrick. Mtandao wa The Sun unaripoti
Mkataba wa kiungo huyo wa United mwenye umri wa miaka 35 unakamilika mwisho wa msimu huku kukiwa na kila dalili za kocha Jose Mourinho kutotaka kuendelea kuwa na kiungo huyo Muingereza.
Arsene Wenger yupo kwenye harakati za kuiongeza nguvu safu yake ya kiungo na ana mpango wa kumrudisha Carrick London Kaskazini ambapo mara ya kwanza kabla ya kiujiunga United alikuwa akichezea kwa wapinzani wao, Tottenham.