Menu

ZIDANE APANIA KUMG’OA CESC FABREGAS KUTOKA CHELSEA

Imeripotiwa kwamba Real Madrid wanafikiria kumsajili kiungo wa Chelsea Cecs Fabregas uhamisho wa majira ya joto.

Muhispania huyo amekabiliwa na wakati mgumu kupata namba kikosi cha kwanza Chelsea chini ya bosi wake Antonio Conte msimu huu, akiwa ameanza mechi tano tu Ligi Kuu Uingereza, 10 akitokea benchi.

Kiungo huyo alikulia kwenye kikosi cha vijana cha Barcelona na alirejea Camp Nou akitokea Arsenal 2011 kabla ya kutua Darajani Stamford miaka mitatu baadaye.

Kwa mujibu wa Diario Gol, bosi wa Real Madrid Zinedine Zidane anafikiria kumsajili Fabregas kwani anataka kuunda safu bora ya kiungo yenye ubunifu hasa ukizingatia mchezaji huyo ana vinasaba vya Barcelona.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 ametwaa mataji matano, ikiwa ni pamoja na lile la La Liga akiwa na miamba wa Catalan.

Comments

comments

Please follow & like us

Video

Tweets