Menu

MASHABIKI SIMBA WAMUWEKA HAJI MANARA KITIMOTO

Klabu ya Simba imeanza utaratibu wa kuwa na mahojiano na viongozi wa klabu hiyo ambapo katika mahojiano hayo, viongozi hao hujibu maswali mbalimbali yanayoulizwa na mashabiki wa klabu hiyo.

Baada ya wiki iliyopita kuwa na mazungumzo na makamu wa Rais wa klabu hiyo ndugu Godfrey Nyange Kaburu ambaye alitoa uhakika kwa mashabiki kuwa msimu ujao mshambuliaji Emmanuel okwi atarejea msimbazi, wiki hii imekuwa ni zamu ya Haji Manara.

Manara ambaye Msemaji Mkuu wa klabu hiyo anatakiwa kujibu maswali kadhaa kutoka kwa mashabiki hao ambao wamekuwa wakituma maswali yao kwenye ukurasa wa facebook wa klabu hiyo na App maalumu ambayo inapatikatikana Google Play.

Moja ya maswali ambayo yameulizwa kwa wingi ni pamoja na suala la maendeleo ya uwanja wa mazoezi wa Bunju pamoja na lile la kumuuzia hisa Mohamed Dewji wakitaka kujua limefikia wapi.

 

Una swali gani kwa Haji Manara?

Comments

comments

Please follow & like us

Video

Tweets