Menu

HAWA NDIO VIUNGO WANNE WAZAWA WANAOWEZA KUTIBU TATIZO SUGU LA KIUNGO MKABAJI YANGA

Klabu ya Yanga, kwa miaka ya hivi karibuni wamekuwa wakihaha kupata kiungo mkabaji bora mwenye uwezo wa kuilinda timu vizuri pindi wanapo shambuliwa hasa kwenye mashindano ya kimataifa.

Tangu kuondoka kwa Athumani Idd Chuji na Frank Domayo ndani ya Yanga, wameshapita viungo wengi ambao wameshindwa kufikia hata nusu ya ubora wa viungo hao, wachezaji kama Twite, Makapu, Pato Ngonyani, Kelvin Yondani wamejaribu kucheza kwenye eneo hili bila mafanikio yeyote.

Mzambia Justin Zulu naye ameonekana hawezi kutatua tatizo la kiungo mkabaji baada ya kiwango chake kutowavutia wengi hivyo klabu imefikiria kuachana nae mwishoni mwa msimu na kusajili nyota mwingine mwenye uwezo mkubwa kwenye nafasi hiyo.

Hawa ni aina ya viungo wakabaji ambao wanahitajika kwa sasa ndani ya klabu ya Yanga

HIMID MAO

Ndiye kiungo bora mkabaji kwa sasa kwenye Ligi Kuu Bara, Himid Mao ni mzuri kwenye kulinda safu yake ya ulinzi vizuri pindi inaposhambuliwa, amekuwa akifanya kazi kubwa uwanjani ya kupokonya mipira muda wote wa mchezo bila kuchoka.

Akitua ndani ya Jangwani ataleta uwiano mzuri kikosini na kuwafanya kina Kamusoko kuwa huru kushambulia muda wote.

JONAS MKUDE

Kiungo huyo wa Simba na timu ya taifa stars anaweza kutatua tatizo la kiungo mkabaji ndani ya Yanga kama wakifanikiwa kuipata saini yake, ni hodari kwenye kuituliza timu na kuziba njia za timu pinzani halikadhalika ni hodari kwa kupiga pasi sahihi fupi na ndefu.

Mkude ni aina ya mchezaji anayehitajika Yanga kwa sasa kwa sababu ni kiungo anayetimiza majukumu yake vizuri kwenye eneo la kati.

KENNY ALLY

Hakuna ubishi, Keny Ally ni aina ya kiungo mkabaji ambao klabu kubwa zote zinapenda kuwa naye msimu ujao wa Ligi Kuu. Kwa muda sasa Yanga wamekuwa wakiuliza bei yake kwa Mbeya City.

Uhodari wake wa kutibua mipango ya wapinzani na uwezo mkubwa wa kufunga kwa mashuti ya mbali kumemfanya kuwa mmoja wa viungo watatu bora kwenye eneo la ulinzi.

FRANK DOMAYO

Alifanya kazi nzuri ndani ya Yanga kabla ajatimkia kwa waoka mikate wa Azam, tangu kuondoka kwake Jangwani kumeifanya klabu hiyo kuyumba kwenye eneo hilo, Yanga bado wana nafasi ya kumrudisha Domayo kwani bado uwezo wake haujapote.

 Chanzo: Goal

Comments

comments

Please follow & like us

Video

Tweets