Menu

KOCHA WA BURUNDI AMPA USHAURI WA BURE OMOG KUHUSU MAVUGO

Kocha mkuu wa Burundi Alain Oliver Niyungeko amesema klabu ya Simba inatakiwa kumpa muda zaidi mshambuliaji wao Laudit Mavugo ili wavune mambo mazuri kutoka kwa nyota huyo raia wa Burundi.

Kocha huyo ambaye alikuja nchini kucheza mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Taifa Stars mechi iliyomalizika kwa Burundi kunyukwa 2-1 alisema

“Mavugo ni mshambuliaji mwenye uwezo mkubwa, aliwahi kuwa mfungaji bora kwenye ligi ya Burundi. Hata kwenye timu ya taifa amekua akifanya vizuri pia.”

“Unapojiunga na timu mpya kwenye ligi mpya wakati mwingine unahitaji muda ili kuzoea, unapokutana na wachezaji wapya kocha mpya na falsafa mpya wakati mwingine inakua vigumu kufanya vizuri mapema hivyo inabidi upate muda wa kuzoea.”

Mavugo alianza kwa kufanya vizuri kwenye mechi za awali baada ya kujiunga na Simba halafu akapotea na akaanza kuwekwa benchi lakini baadae akaibuka tena na kuanza kufanya vizuri na kurudi kwenye kikosi cha kwanza cha kocha Joseph Omog.

Goli pekee la Burundi kwenye mchezo dhidi ya Stars lilifungwa na Mavugo kipindi cha pili.

Comments

comments

Please follow & like us

Video

Tweets