Menu

MO AZIUNGANISHA SIMBA NA JUVENTUS; HIVI NDIVYO SIMBA ITAKAVYONEEMEKA.

Ziara ya mwanachama bilionea wa klabu ya Simba Mohamed Dewji kwenye klabu kongwe ya Juventus haikuwa ya kazi bure. Hivyo ndivyo unavyoweza kusema.

Wiki iliyopita tajiri huyo ambaye ana mpango wa kuinunua klabu hiyo ka hisa asilimia 51 alikuwa jijini Turin yalipo makao makuu ya klabu kongwe nchini Italia na barani ulaya kwa ujumla ya Juventus akipiga picha na baadhi ya viongozi wakubwa wa klabu hiyo

Taarifa kutoka kwenye gazeti la Mwana Soka ambalo ni mahususi kwa ajili ya habari za Simba zinadai kuwa kuna mpango wa klabu ya Simba kuungana na mabingwa hao wa ligi ya Italia na kufanya nao kazi pamoja ikiwa ni pamoja na kuwekeza katika timu ya kikosi cha pili cha Simba ambacho kitakuwa kikilelewa na klabu hiyo ya Juventus

Sambamba na hilo, taarifa zinaeleza kuwa klabu hiyo ya Juventus itaisaidia Simba katika ujenzi wa uwanja wake na kituo cha michezo katika eneo la bunju huku pia wachezaji wa kikosi cha timu ya wakubwa watakuwa wakipata nafasi ya kwenda kufanya majaribio katika vilabu mbalimbali vya soka barani Ulaya kupitia klabu ya Juventus.

Mbali na hayo yote pia, kuna makubaliano kuwa klabu hiyo ya Simba itakwenda kupiga kambi katika dimba la Juventus ikiwa ni fursa kwa wachezaji hao kujifunza zaidi.

Chanzo: MwanaSoka

Comments

comments

Please follow & like us

Video

Tweets