Menu

NYOTA HAWA 11 WAPO HATARINI KUPITIWA NA PANGA LA LWANDAMINA JANGWANI

Kocha wa mkuu wa klabu ya Yanga, George Lwandamina anatarajia kupitisha panga kwenye kikosi chake kwa kuondoa majina ya wachezaji 11 mwishoni mwa msimu katika harakati za kuunda upya timu hiyo.

Panga hilo linatokana na ripoti itakayowasilishwa na kocha huyo kwa uongozi huku ikiwa na baadhi ya wachezaji wenye majina makubwa.

Taarifa kutoka kwa mtu wa ndani wa klabu ya Yanga zinasema kuwa miongoni mwa wachezaji walio katika hatihati ya kuachwa ni pamoja na wachezaji wa kigeni ambao wanamaliza mikataba yao mwishonui mwa msimu huu na hawana mpango wa kuendelea kuichezea timu hiyo ikiwa ni pamoja na Vincent Bossou, Haruna Niyonzima na Donald Ngoma.

Wachezaji wazawa ambao mikataba yao inamalizika na hawana dalili za kuongezwa kutokana na viwango vyao kuporomoka ni pamoja na Malimi Busungu, Matheo Anthony na Oscar Joshua

Wachezaji Thaban Kamusoko, Amisi Tambwe, Mwinyi Haji, Nadir Haroub na kipa Deogratious Munishi mikataba yao inamalizika mwishoni mwa msimu huu na hakuna dalili za kuongeza

Wengine ambao bado wana mikataba na klabu hiyo lakini wanaweza kutolewa kwa mkopo ni pamoja na Geofrey Mwashiuya, Pato Ngonyani, Deus Kaseke, Said Juma  na Vincent Andrew.

Aidha kuna sekeseke linaendelea klabu hapo kuhusiana na golikipa Ali Mustapha ambaye ameugawa uongozi huku wengine wakitaka abaki na wengine wakitaka aondoke kwa madai ya kutokuwa na imani naye.

Chanzo: Gazeti la Burudani

Comments

comments

Please follow & like us

Video

Tweets