Menu

HILI NDILO TAMKO LA KLABU YA SIMBA JUU YA NYASI ZAO BANDIA ZILIZOTAKA KUPIGWA BEI HAPO JANA

Habari kubwa iliyokuwa imetawala vyombo vya habari kwenye soka ni ile ya Mamlaka ya Mapato Tanzania kutangaza kupiga mnada nyasi bandia za klabu ya Simba ambazo hazijalipiwa ushuru.

Hata hivyo mapema asububhi ya leo, Klabu ya Simba imeweza kutoa tamko juu ya sakata hilo kupitia kwenye akaunti yao ya mtandao wa Facebook ambapo wameandika haya:

“Klabu ya Simba inakiri kudaiwa na Mamlaka ya mapato nchini “TRA” kodi za nyasi bandia na juhudi za kupata msamaha wa kodi hiyo kiuhalisia umeshindikana.

Klabu inafanya juhudi zote kuhakikisha inalipa kodi hiyo kwa wakati baada ya kuomba kuongezewa muda wa kulipa na TRA, pia klabu tunaishukuru sana mamlaka hiyo kwa kutuvumilia na kutupa muda zaidi.

Kwa sasa tunawaomba wanachama na washabiki wetu kujikita kwenye mechi zetu muhimu za kanda ya ziwa na kupuuza maneno ya mitandaoni yenye lengo kwa klabu yetu”.

Comments

comments

Please follow & like us

Video

Tweets