Menu

TETESI: SAMATTA AWINDWA LIGI YA UJERUMANI

Mtandao wa Soka360 unaripoti kuwa vilabu vitatu vya Ligi ya Ujerumani, maarufu kama Bundesliga vinamfuatilia kwa ukaribu mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta.

Kwa mujibu wa wakala anayeishi Ubelgiji makachero wa timu za  Wolfsburg, Hamburger SV na  Borussia Mönchengladbach  wamekuwa wakimfuatilia Samatta anayetajwa kuwekewa thamani ya euro milioni 10.

Klabu ya Genk inasemekana iko tayari kumuachi Samatta mwenye mkataba hadi mwaka 2020 kwa dau lisilopungua euro milioni 10 licha ya kumnunua kwa Euro 800,000 kutoka klabu ya TP Mazembe mwanzoni mwa mwaka jana.

 

Comments

comments

Please follow & like us

Video

Tweets