Menu

Sera ya Faragha

Sera ya Faragha ya Michezo Plus.

Unapotumia huduma za Michezo Plus  unatuamini na maelezo na faragha yako. Sera hii imekusudia kukusaidia kuuelewa taarifa mbalimbali tunazokusanya, sababu za kukusanya na tunachofanya nayo.Sera hii ni muhimu; tunatumaini utatenga muda kuisoma kwa makini na kuielewa, kama kuna ambacho hujaelewa, tafadhali tembelea ukurasa hapa na kuomba kupatiwa maelezo ya ziada.Ni vyema pia kukumbuka kuwa unaweza kupata na kutumia vidhibiti data, kudhibiti maelezo yako na kulinda faragha na usalama wako.

Sera ya Faragha ya Michezo Plus inaeleza  kwa kina;

 • Maelezo tunayoyakusanya na sababu za kufanya hivyo.
 • Jinsi tunavyoyatumia maelezo hayo.

Tumejaribu kuifanya rahisi iwezekanavyo, lakini kama hujazoea maneno ya kitaamu kama vile vidakuzi, anwani za IP, lebo za pikseli na vivinjari, basi soma kuhusu istilahi hizi muhimu kwanza. Kwa msaada wa kuhusu istalahi mbalimbali za kiteknolojia, tafadhali tembelea ukurasa huu unaotolewa kwa hisani ya mtandao wa Google.Faragha yako ni muhimu kwetu. Ili uweze kutumia huduma zetu kwa uhuru, tafadhali chukua nafasi ujifahamishe kuhusu Sera yetu ya faragha.

Maelezo tunayokusanya

Ili kukupa huduma bora zaidi, Michezo Plus hukusanya baadhi ya taarifa za watumiaji wake. Taarifa tunazokusanya zinagawanyika katika makundi mawili. La kwanza ni taarifa unazotupa mwenyewe unapojiunga na huduma zetu kama vile, barua pepe za kila mwezi, huduma zetu za SMS na WhatsApp.Kundi la pili la taarifa tunazokusanya ni kwa kutokana na matumizi yako ya huduma zetu. Tunakusanya maelezo kuhusu huduma ambazo unatumia, njia unazotumia na jinsi unavyozitumia. Maelezo hayo ni pamoja na:

Maelezo juu ya kifaa unachotumia.

Tunakusanya maelezo yanayohusu kifaa unachotumia kupata huduma zetu. Maelezo hayo ni kama vile aina ya kifaa hicho, toleo la mfumo wa uendeshaji, vitambulishi vya kipekee vya kifaa, na maelezo ya mtandao wa simu ikiwa ni pamoja na nambari ya simu.

Maelezo ya kumbukumbu

Kila unapotumia huduma zetu au kutazama maudhui yaliyotolewa na Michezo Plus tunakusanya na kuhifadhi maelezo mengine kiotomatiki kwenye kumbukumbu zetu. Maelezo hayo ni pamoja na:

 • Anwani ya Itifaki Wavuti (IP). Kila kifaa kilichounganishwa kwenye Intaneti kimetawazwa nambari inayojulikana kama anwani ya itifaki ya Intaneti (IP). Kwa kawaida nambari hizi hutawazwa katika vikundi vya kijiografia. Mara nyingi anwani ya IP inaweza kutumiwa kutambua kifaa kinaunganishwa kutoka eneo gani kwenye Intaneti.
 • Maelezo ya matukio kwenye kifaa kama kukwama kwa kifaa, utendakazi wa mfumo, mipangilio ya maunzi, aina ya kivinjari, lugha ya kivinjari, tarehe na saa ya ombi lako na URL marejeleo.
 • Vidakuzi ambavyo vinaweza kutambulisha kivinjari kwa njia ya kipekee. Kidakuzi ni faili ndogo iliyo na msururu wa herufi inayotumwa kwa kompyuta yako unapotembelea tovuti fulani. Unapotembelea tovuti hiyo tena, kidakuzi huruhusu tovuti hiyo itambue kivinjari chako. Vidakuzi vinaweza kuhifadhi mapendeleo ya mtumiaji na maelezo mengine. Unaweza kuweka kivinjari chako upya ili kisikubali vidakuzi vyovyote au kionyeshe kidakuzi kinapotumwa. Hata hivyo, vipengee vingine vya tovuti au huduma huenda visifanye kazi vizuri bila vidakuzi. Teknolojia nyingine hutumiwa kwa malengo sawa kama kidakuzi kwenye mifumo mengine ambapo vidakuzi havipatikani au havitumiki, kama vile Kitambulisho cha Utangazaji kinachopatikana kwenye vifaa vya mkononi vya Android.

Maelezo ya eneo

Wakati unapotumia huduma za Michezo Plus, tunaweza kukusanya na kuchakata maelezo kuhusu eneo lako halisi. Tunatumia teknolojia mbalimbali kubainisha eneo, ikiwa ni pamoja na anwani ya IP na vidakuzi (angalia maelezo hapo juu).

Vidakuzi na teknolojia sawa

 • Sisi na washirika wetu hutumia teknolojia mbalimbali kukusanya na kuhifadhi maelezo wakati unapotembelea na kutumia huduma zetu. Kufanikisha hili, tunatumia vidakuzi na teknolojia sawa ili kutambua kivinjari au kifaa chako.
 • Tunatumia pia teknolojia hizi kukusanya na kuhifadhi maelezo wakati unapowasiliana na huduma tunazotoa kwa washirika wetu, kama vile huduma za matangazo au vipengee vya Michezo Plus vinavyoweza kuonekana kwenye tovuti nyingine.

 Jinsi tunavyotumia maelezo tunayoyakusanya

Tunatumia maelezo tunayokusanya kwenye huduma zetu zote kutoa, kudumisha, kulinda na kuboresha huduma hizi, kubuni nyingine mpya, na kulinda Michezo Plus na wateja wetu. Pia tunatumia maelezo haya kukupa maudhui ya kukufaa – kama vile matangazo.Tunatumia maelezo yaliyokusanywa kutokana na vidakuzi na teknolojia zingine, kama lebo za pikseli, ili kuboresha matumizi yako na ubora wa kijumla wa huduma zetu.  Mifumo yetu ya kiotomatiki huchanganua maudhui yako ili kukupa kibinafsi vipengele husika vya bidhaa, kama vile ujumbe wa barua pepe, SMS au WhatsApp uliobinafsishwa na utangazaji ulio binafsishwa.

Kabla ya kutumia maelezo yako tunayokusanya kwa madhumuni mengine tofauti na yaliyoanishwa kwenye sera hii ya faragha, tutaomba ruhusa kwako.

Sera yetu ya uwazi na chaguo la mteja.

Tunatambua kuwa, kila mmoja wetu ana mtazamo na msimamo tofauti juu ya faragha.  Lengo letu ni kuwa na uwazi kuhusu ni maelezo yapi tunayoyakusanya, ili uwezo kufanya uamuzi wa maana kuhusu jinsi yanavyotumika. Kwa mfano, unaweza:

 • Kukagua na kusahihisha vidhibiti vyako vya shughuli za Michezo Plus ili uamue ni aina gani ya taarifa upo tayari tuzikusanye unapotumia huduma za Michezo Plus.
 • Tazama na ubadilishe mapendeleo yako kuhusu matangazo kutoka Michezo Plus yanayoonyeshwa kwako kwenye tovuti ya Michezo Plus.
 • Unaweza pia kutoruhusi vidakuzi vyovyote vya Michezo Plus kwenye kipitiaji chako kwa kuzuia kuki zote pamoja na kuki zinazohusiana na huduma zetu.
 • Hata hivyo, ni muhimu kukumbuka kwamba huduma zetu nyingi zinaweza zisifanye kazi vizuri kama kuki zako zimeondolewa uwezo.

 Maelezo tunayoshirikisha

Kwa kawaida, maelezo na taarifa zote tunazokusanya zinatumiwa na Michezo Plus pekee. Hatushirikishi maelezo ya kibinafsi na kampuni, mashirika, na watu binafsi nje ya Michezo Plus isipokuwa mojawapo ya hali zifuatazo itokee:

Kwa idhini yako

Tutashirikisha maelezo ya kibinafsi na kampuni, mashirika, na watu wa nje ya Michezo Plus tukiwa na idhini yako ya kufanya hivyo. Tunahitaji kibali cha uamuzi wa kuingia cha kushirikisha maelezo yoyote nyeti ya kibinafsi.

Kwa mchakato wa nje

Tunatoa maelezo ya kibinafsi kwa washirika wetu wadogo au biashara zingine tunazoamini au watu ili kuichakata kwa niaba yetu, kulingana na maagizo yetu na kwa kufuata Sera yetu ya Faragha na hatua zingine zozote zinazofaa za faragha na usalama.

Kwa sababu za kisheria

Tutashirikisha maelezo ya kibinafsi na makampuni, mashirika au watu walioko nje ya Michezo Plus ikiwa tuna imani kwamba ufikiaji, matumizi, uhifadhi au ufichuzi wa maelezo hayo ni muhimu ili:

 • Kutimiza sheria yoyote husika, masharti, mchakato wa kisheria au ombi linaloweza kutekelezwa la kiserikali
 • Kutekeleza masharti husika ya huduma, ikiwa ni pamoja na uchungzi wa ukiukaji unaowezekana kutokea.
 • Kugundua, kuzuia, au kushughulikia ulaghai, masuala ya usalama au kiufundi.
 • Kulinda dhidi ya madhara ya haki, mali au usalama wa michezo plus, watumiaji wetu au umma kama inavyotakikana au kuruhusiwa na sheria.

Usalama wa maelezo

Tunafanya bidii kulinda Michezo Plus na watumiaji wetu dhidi ya ufikiaji ambao haujaidhinishwa au mabadiliko yasiyoidhinishwa, uchakachuaji haramu au uharibifu wa maelezo tuliyoweka.  Taarifa zinazokusanywa zipo salama kwenye mitambo yetu yenye kutumia teknolojia ya hali ya juu.

Mabadiliko

Sera yetu ya Faragaha inaweza kubadilika mara kwa mara. Hatutapunguza haki zako chini ya Sera ya Faragha hii bila idhini yako dhahiri. Tutachapisha mabadiliko yoyote ya sera ya faragha kwenye ukurasa huu na, kama mabadiliko ni muhimu, tutatoa taarifa inayoonekana zaidi (inayojumuisha, kwa huduma fulani, taarifa ya barua pepe ya mabadiliko ya sera ya faragha). Pia tutaweka toleo za awali za Sera ya Faragha hii katika kumbukumbu kwa tathmini yako.

Please follow & like us

Video

Tweets