Menu

Vigezo na Masharti

Vigezo na Masharti ya Michezo Plus

Karibu sana Michezo Plus!

Asante kwa kutumia huduma zetu. Huduma zinatolewa na Michezo Plus zinasimamiwa na KwanzaMedia.Vigezo na masharti vyote vinasimamiwa na Sheria za Jamhuri ya Tanzania. Kesi zote zinazohusiana na Michezo Plus na washirika wake ni lazima ziwakilishwe kwenye mahakama za Tanzania na si kwingineko. Kwa kutumia Huduma zetu, moja kwa moja unakubaliana na vigezo na masharti haya. Tafadhali yasome kwa makini na kuyaelewa. Kama kuna swali au unahitaji maelezo ya ziada, tafadhali tembelea ukurasa huu na kuwasilisha ombi lako.Ili kutumia huduma zetu, ni lazima ufuate sera zozote zinazotolewa kwako na unakubaliana na Sera yetu ya faragha. Vigezo na masharti ya kutumia huduma zetu ni kama ifuatavyo;

 • Usitumie Huduma zetu vibaya. Kwa mfano, usivuruge huduma zetu au kujaribu kuzifikia kwa kutumia mbinu nyingine isipokuwa kiolesura na maagizo tunayotoa.
 • Unaweza kutumia huduma zetu kama inavyoruhusiwa kisheria tu, zikiwemo sheria na kanuni husika za kudhibiti maudhui.
 • Tunaweza kusimamisha au kusitisha utoaji wa huduma zetu kwako kama hutafuata masharti au sera zetu au kama tunachunguza mwenendo mbaya tunaoshuku.
 • Kutumia huduma zetu hakukupi umiliki wa hakimiliki zozote katika huduma zetu au maudhui unayoyapata.
 • Huwezi kutumia maudhui kutoka kwenye Huduma zetu bila ruhusa ya ya maandishi ya Michezo Plus au umeruhusiwa vinginevyo kisheria kufanya hivyo.
 • Masharti haya hayakupi haki ya kutumia maudhui, rajamu au nembo zozote zinazotumiwa katika huduma zetu.
 • Usiondoe, usifute wala usibadilishe taarifa zozote za kisheria zinazoonyeshwa ndani ya au pamoja na huduma zetu.
 • Huduma zetu huonyesha maudhui mengine ambayo si ya Michezo Plus. Maudhui hayo ni wajibu wa yule anayeyatoa peke yake.
 • Tunaweza kutathmini maudhui ili kuamua kama ni kinyume cha sheria au yanakiuka sera zetu, na tunaweza kuondoa au kukataa kuyaonyesha maudhui tunayoamini yanakiuka sera zetu au sheria. Lakini hiyo haimaanishi ya kwamba tunatathmini maudhui kila wakati, kwa hivyo tafadhali usidhani kuwa tunafanya hivyo.
 • Kuhusiana na matumizi yako ya huduma, tunaweza kukutumia matangazo ya arafi za huduma, ujumbe wa usimamizi na maelezo mengine. Unaweza kuamua kujiondoa kwenye baadhi ya mawasiliano hayo.
 • Baadhi ya huduma zetu zinapatikana kwenye vifaa vya mkononi. Usitumie huduma kama hizo katika njia ambayo inakutatiza na kukuzuia kutii sheria za trafiki au za usalama.

Ulinzi wa Faragha na Hakimiliki

Sera za faragha za Michezo Plus huelezea tunavyokusanya na kutumia taarifa zako binafsi na kulinda faragha yako unapotumia huduma zetu. Kwa kutumia huduma zetu, unakubali kwamba MichezoPlus inaweza kutumia taarifa hiyo kulingana na sera zetu za faragha.Hairuhusiwi kwa namna yoyote kunakili au kusambaza maudhui yaliyo kwenye tovuti hii. Kufanya hivyo ni kinyume na sheria, Michezo Plus wana haki ya kukuchukulia hatua za kisheria.Huruhusiwi kunakili, kubadilisha, kusambaza, kuuza au kukodisha sehemu yoyote ya huduma zetu au programu zilizojumuishwa, isipokuwa sheria iwe inazuia vikwazo hivyo au una ruhusa yetu kimaandishi.

Kubadilisha na Kukatisha Huduma zetu.

Tunabadilisha na kuboresha Huduma zetu kila wakati. Tunaweza kuongeza au kuondoa utendakazi au vipengele, na tunaweza kusimamisha au kusitisha Huduma kabisa.Unaweza kuacha kutumia Huduma zetu wakati wowote, ingawa tutasikitika kukupoteza. MichezoPlus inaweza kuacha kukupa huduma, inaweza pia kuongeza au kuweka mipaka mipya kwa huduma zetu wakati wowote.

Hakikisho na Kanusho Zetu

Tunatoa huduma zetu kwa kutumia kiwango cha ujuzi na uangalifu wa kibiashara unaofaa na tuna tumaini utafurahia kuzitumia. Lakini kuna mambo fulani ambayo hatuahidi kuhusu huduma zetu.

Isipokuwa vile ilivyodhihirishwa katika masharti haya au masharti ya ziada, Michezo Plus, waletaji au wasambazaji wake hawatoi ahadi yoyote mahsusi kuhusu huduma. Kwa mfano, hatuweki ahadi zozote kuhusu maudhui ndani ya huduma, kazi mahususi ya huduma, au uthabiti wao, upatikanaji, au uwezo wa kukutimizia mahitaji yako. Tunatoa huduma “kama ilivyo”

Baadhi ya haki za kisheria, zilitoa dhamana fulani, kama dhamana ya kuwa katika hali nzuri ya biashara, ufao wake kwa kazi fulani na isiyokiukwa. Tunatoa dhamana zote ila tu kwa kiasi hicho kilichoruhusiwa na sheria.

Dhima ya Huduma zetu

Kama imeruhusiwa kisheria, MichezoPlus, na waletaji na wasambazaji wake, hawatawajibika kwa upotezaji wa faida, mapato, au data, fedha; au uharibifu usio wa moja kwa moja,maalum, wa tukio,wa kipekee, au wa adhabu.Mpaka kwa kiwango kinachokubaliwa kisheria, jumla ya dhima ya Michezo Plus, na waletaji na wasambazaji wake, kwa madai yoyote chini ya masharti haya, pamoja na dhamana zilizodokezwa, haitazidi kiwango ulichotulipa ili kutumia huduma (au, tukichagua, kukupatia huduma tena).Katika kesi zote, Michezo Plus na waletaji wake na wasambazaji, hawatawajibika kwa uharibifu au hasara ambayo haiwezi kutarajiwa.

Matumizi ya kibiashara ya Huduma zetu

Kama unatumia huduma zetu kwa niaba ya biashara, biashara hiyo inayakubali masharti haya. Itaichukulia MichezoPlus kuwa bila hatia na itaifidia pamoja na washirika wake, maafisa, mawakala, na wafanyakazi kutokana na madai yoyote, mashtaka au kesi kutokana na au kuhusiana na matumizi ya huduma au ukiukaji wa masharti haya, ikiwa ni pamoja na dhima au gharama yoyote kutokana na madai, hasara, uharibifu, mashtaka, hukumu, gharama za mashtaka na ada za wakili.

Kuhusu Masharti haya

Tunaweza kubadilisha masharti haya au masharti ya ziada yanayotumika kwa huduma, kwa mfano, kuonyesha mabadiliko katika sheria au mabadiliko katika huduma zetu. Inafaa uangalie masharti haya mara kwa mara.Tutaweka taarifa za marekebisho ya masharti haya kwenye ukurasa huu. Tutaweka taarifa ya masharti ya ziada yaliyorekebishwa katika Huduma husika.Mabadiliko hayatatekelezwa kwa wakati uliopita na yataanza kufanya kazi baada ya angalau siku kumi na nne baada ya kuchapishwa. Lakini, mabadiliko yanayoshughulikia utendakazi mpya wa huduma au mabadiliko yaliyofanywa kwa sababu za kisheria yatatumika mara moja. Kama hukubaliani na masharti yaliyobadilishwa ya huduma fulani, unafaa uache kutumia huduma hiyo.Kama kuna ukinzani kati ya masharti haya na masharti ya ziada, masharti ya ziada yatadhibiti ukinzani huo.Masharti haya yadhibiti uhusiano kati yako na MichezoPlus. Hayaleti haki zozote kufaidi mhusika mwingine.Kama hutii masharti haya, na hatuchukui hatua mara moja, hii haimaanishi ya kwamba tunasalimisha haki zozote ambazo tunazo (kama vile kuchukua hatua baadaye).

 

Please follow & like us

Video

Tweets